2 Timotheo UTANGULIZI - Swahili Revised Union Version DC

UTANGULIZIKuhusu huyu Timotheo tazama utangulizi kwa Waraka wa Kwanza kwa Timotheo. Inaaminika kuwa baada ya Paulo kuandika Waraka wa kwanza kwa Timotheo alitembelea baadhi ya Makanisa (2 Tim 4:13,20) ndipo aliposhikwa akafungwa na baadaye akapelekwa Rumi tena akiwa mfungwa. Akiwa kule Rumi aliandika Waraka huu wa Pili kwa Timotheo (1:18; 2:9).Tofauti na Nyaraka nyingine zote za Paulo, Waraka huu karibu wote unamlenga Timotheo binafsi. Hata hivyo, kama zile Nyaraka za kichungaji, huu nao unawahusu pia viongozi wa kanisa la Kikristo. Mafundisho yake yanafaa sana kwa hao viongozi katika kuendelea kuishi vilivyo hapa duniani. Timotheo anaonekana katika Waraka huu kama mtu mwenye madaraka juu ya jumuiya kadhaa za kanisa na anashauriwa awatie moyo na kuwakinga na mitindo yenye kuangamiza imani ya Kikristo kutoka nje na ndani. Anatakiwa kukiweka motomoto kipaji cha Mungu kilicho ndani yake (1:3-7), asiwe na haya kumshuhudia Kristo Bwana (1:8-18) na kushiriki sehemu yake ya mateso kama askari hodari wa Kristo (2:1-13).
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help