1 1 Tim 6:3; 2 Tim 1:13 Lakini wewe, nena mambo yanayoambatana na mafundisho mema;
21 Tim 5:1 ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika subira.
31 Tim 3:11 Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wanaofundisha yaliyo mema;
4ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;
5Efe 5:22 na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.
6Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi;
71 Tim 4:12; 1 Pet 5:3 katika mambo yote ukijionesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionesha usahihi na ustahivu,
81 Pet 2:15 na maneno yafaayo yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.
9 Efe 6:5; 1 Tim 6:1; 1 Pet 2:18 Watumwa na wawatii bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wakaidi,
10Tit 1:3 wasiwe wezi; bali wauoneshe uaminifu mwema wote, ili wayapambe mafundisho ya Mungu aliye Mwokozi wetu katika mambo yote.
11Maana neema ya Mungu iwaokoao wanadamu wote imefunuliwa;
12Efe 1:4; 1 Yoh 2:16 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
131 Kor 1:7; Rum 5:2; Flp 3:20 tukilitazamia tumaini lenye baraka na kufunuliwa kwa utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
14Kut 19:5; Kum 4:20; 7:6; 14:2; Zab 130:8; 1 Pet 2:9; 3:13; Gal 1:4; 1 Tim 2:6; Efe 2:10; Eze 37:23 ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wake mwenyewe walio na bidii katika matendo mema.
15 1 Tim 4:12 Nena mambo hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.