1 1 Sam 2:21; Mwa 17:19; 18:10; Gal 4:23 BWANA akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema.
2Ebr 11:11; Mdo 7:8 Sara akapata mimba akamzalia Abrahamu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu.
3Mwa 17:19 Abrahamu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia.
4Mwa 17:12; Mdo 7:8 Abrahamu akamtahiri Isaka mwanawe, alipokuwa mwenye siku nane, kama Mungu alivyomwamuru.
5Naye Abrahamu alikuwa mtu wa miaka mia moja, alipozaliwa mwana wake Isaka.
6Zab 126:2; Isa 54:1; Lk 1:14,58 Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami.
7Mwa 18:11 Akasema, Ni nani angemwambia Abrahamu, Sara atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake.
Hajiri na Ishmaeli wafukuzwa8Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Abrahamu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.
9Mwa 16:1,4,15; Gal 4:29 Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Abrahamu, anafanya dhihaka.
10Gal 4:29-30; Mwa 25:6; 36:6,7 Kwa hiyo akamwambia Abrahamu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.
11Mwa 17:18 Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Abrahamu, kwa ajili ya mwanawe.
12Rum 9:7; Ebr 11:18 Mungu akamwambia Abrahamu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.
13Mwa 16:10; 17:20; 25:12 Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako.
14 Yn 8:35 Abrahamu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akamtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.
15Hes 20:5; Zab 63:1 Yale maji yalipoisha katika kiriba, Hajiri akamlaza kijana kichakani.
16Mwa 44:34 Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia.
17Kut 3:7; 2 Fal 13:4,23 Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.
18Mwa 21:13; 25:12; Amu 8:24 Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.
19Hes 22:31; 2 Fal 6:17; Lk 24:16 Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.
20 Mwa 16:12; 39:2,3 Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
21Mwa 24:4; 20:2; 26:28; Isa 8:10 Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.
Abrahamu na Abimeleki wawekeana agano22 Mwa 26:26 Ikawa wakati ule Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakamwambia Abrahamu, wakinena, Mungu yu pamoja nawe katika yote unayotenda.
23Yos 2:12; 1 Sam 24:21 Basi sasa uniapie kwa Mungu, ya kuwa hutanitenda hila, wala mwanangu, wala mjukuu wangu, lakini kwa kadiri ya fadhili niliyokutendea utanitendea mimi, na nchi hii ambayo umetembea ndani yake.
24Abrahamu akasema, Nitaapa.
25 Mwa 26:15-22 Kisha Abrahamu akamlaumu Abimeleki kwa sababu ya kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki wamemnyang'anya.
26Abimeleki akasema, Mimi sijui ni nani aliyetenda neno hili, wala hukuniambia, wala sikusikia habari hii ila leo tu.
27Mwa 26:28-31 Abrahamu akatwaa kondoo na ng'ombe akampa Abimeleki, na hao wawili wakafanya mapatano.
28Abrahamu akawaweka wana-kondoo saba wa kike peke yao.
29Mwa 33:8 Abimeleki akamwuliza Abrahamu, Hawa wana-kondoo saba majike, uliowaweka, maana yake ni nini?
30Mwa 31:48 Akasema, Hawa wana-kondoo saba majike utawapokea mkononi mwangu, wawe ushuhuda ya kuwa ni mimi niliyekichimba kisima hiki.
31Mwa 26:33 Kwa hiyo akapaita mahali pale Beer-sheba, kwa sababu waliapa huko wote wawili.
32Yos 13:2 Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti.
33Kum 33:27; Zab 9:7; Isa 9:6; Rum 16:26; Ebr 13:8; 1 Tim 1:17; Ufu 10:6 Abrahamu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la BWANA Mungu wa milele.
34Abrahamu akaishi kama mgeni kwa Wafilisti siku nyingi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.