Zaburi 39 - Swahili Revised Union Version DC

Sala ya kutaka hekima na msamahaKwa mwimbishaji: kwa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi.

1 1 Fal 2:4; Mit 4:26,27; Ebr 2:1; Kol 4:5 Nilisema, Nitazitunza njia zangu

Nisije nikakosa kwa ulimi wangu;

Nitajitia lijamu kinywani,

Maadamu mtu mbaya awapo mbele yangu.

2Nilikuwa sisemi, nilinyamaa kimya,

Sina faraja, maumivu yangu yakazidi.

3 Yer 20:9 Moyo wangu ukawa moto ndani yangu,

Na katika kuwaza kwangu moto ukawaka;

Nilisema kwa ulimi wangu,

4BWANA, unijulishe mwisho wangu,

Na idadi ya siku zangu ni ngapi;

Nijue jinsi maisha yangu yalivyo mafupi.

5 Zab 90:4 Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri;

Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako.

Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.

6Kweli, watu wote hupita kama kivuli;

Wao hujisumbua bure tu;

Wanajirundikia mali wala hawajui ni nani atakayeirithi.

7Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana?

Matumaini yangu ni kwako.

8Uniokoe kutoka kwa maasi yangu yote,

Usinifanye niwe wa kulaumiwa na mpumbavu.

9Nimenyamaza, sifumbui kinywa changu,

Maana Wewe ndiwe uliyeyafanya.

10Uniondolee pigo lako;

Kwa mapigo ya mkono wako nimeangamia.

11Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake,

Watowesha uzuri wake kama nondo.

Kila mwanadamu ni ubatili.

12 Law 25:23; 1 Nya 29:15 Ee BWANA, usikie maombi yangu,

Utege sikio lako niliapo,

Usiyapuuze machozi yangu.

Kwa maana mimi ni mgeni wako,

Msafiri kama baba zangu wote.

13 Ayu 10:20,21 Uache kunitazama, ndio nipate kufurahi tena,

Kabla sijafa na kutoweka kabisa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help