1 kwa kuwa tu wengi.
10Akamsihi sana asiwapeleke nje ya nchi ile.
11Na hapo milimani palikuwa na kundi kubwa la nguruwe, wakila.
12Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao.
13Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likateremka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapatao elfu mbili; wakafa baharini.
14Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea.
15Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi la pepo; wakaogopa.
16Na wale waliokuwa wameona waliwaeleza ni mambo gani yaliyompata yule mwenye pepo, na kuhusu nguruwe.
17Wakaanza kumsihi aondoke katika eneo lao.
18Naye alipokuwa akipanda katika mashua, yule aliyekuwa na pepo akamsihi kwamba awe pamoja naye;
19lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Nenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubirie ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu.
20Mk 7:31; Mt 4:25 Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu.
Msichana arudishiwa uhai na mwanamke kuponywa21Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng'ambo katika ile mashua, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari.
22Mt 9:18-26; Lk 8:41-56 Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake,
23Mk 7:32 akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yuko karibu kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi.
24Akaenda pamoja naye; mkutano mkuu wakamfuata, wakimsongasonga.
25Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili,
26na kuvumilia mateso mengi kutoka kwa matabibu wengi, na kugharimiwa mali yake yote aliyokuwa nayo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya.
27Aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake;
28maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.
29Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule.
30Lk 6:19 Mara Yesu, huku akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu?
31Wanafunzi wake wakamwambia, Je! Wawaona makutano wanavyokusongasonga, nawe wasema, Ni nani aliyenigusa?
32Akatazama pande zote ili amwone yule aliyelitenda neno hilo.
33Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza ukweli wote.
34Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, nenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.
35Hata alipokuwa katika kunena, wakaja watu kutoka kwa yule mkuu wa sinagogi, wakisema, Binti yako amekwisha kufa; kwa nini uzidi kumsumbua mwalimu?
36Lakini Yesu, alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu.
37Wala hakumruhusu mtu afuatane naye, ila Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye Yakobo.
38Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo makuu.
39Yn 11:11 Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, bali amelala tu.
40Wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa babaye yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwamo yule kijana.
41Lk 7:14 Akamshika mkono kijana, akamwambia, Talitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka.
42Mara akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata umri wa miaka kumi na miwili. Mara wakashangaa mshangao mkuu.
43Mk 1:44 Akawaonya sana, mtu asijue habari ile; akaamuru apewe chakula.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.