Marko 6 - Swahili Revised Union Version DC

Kukataliwa kwa Yesu Nazareti

1 mia mbili ili tuwape kula?

38Akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame. Walipokwisha kujua wakasema, Mitano, na samaki wawili.

39Akawaagiza wawaketishe wote, vikao vikao, penye majani mabichi.

40Wakaketi safu safu, hapa mia hapa hamsini.

41Mk 7:34 Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandalie; na wale samaki wawili akawagawia wote.

42Wakala wote wakashiba.

43Kum 28:5 Wakaokota vipande vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu kumi na viwili; na vipande vya samaki pia.

44Na walioila ile mikate walikuwa wanaume elfu tano.

Yesu atembea juu ya maji

45 Mt 14:22-36; Yn 6:15-21 Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande mashuani, watangulie kwenda ng'ambo hata Bethsaida, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano.

46Hata alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kuomba.

47Na kulipokuwa jioni mashua ilikuwa katikati ya bahari, na yeye yu peke yake katika nchi kavu.

48Akawaona wakitaabika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa unwakabili; hata ilipopata kama zamu ya nne ya usiku akawaendea, akitembea juu ya bahari; akataka kuwapita.

49Nao walipomwona anatembea juu ya bahari, walidhani ya kuwa ni mzuka, wakapiga yowe,

50kwa kuwa wote walimwona, wakafadhaika. Mara akasema nao, akawaambia, Changamkeni; ni mimi, msiogope.

51Mk 4:39 Akapanda mle katika mashua walimo; upepo ukakoma; wakashangaa sana mioyoni mwao;

52kwa maana hawakufahamu habari za ile mikate, lakini mioyo yao ilikuwa mizito.

Kuwaponya wagonjwa Genesareti

53Hata walipokwisha kuvuka, walifika nchi ya Genesareti, wakatia nanga.

54Nao wakiisha kutoka mashuani, mara watu walimtambua,

55wakaenda mbio, wakizunguka nchi ile yote, wakaanza kuwachukua vitandani waliokuwa wagonjwa, kwenda kila mahali waliposikia kwamba yupo.

56Mk 5:27,28; Mdo 5:15; 19:11,12 Na kila alikokwenda, akiingia vijijini, au mijini, au mashambani, wakawaweka wagonjwa sokoni, wakamsihi waguse angaa pindo la vazi lake; nao wote waliomgusa wakapona.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help