Mwanzo 15 - Swahili Revised Union Version DC

Agano la Mungu na Abramu

1 Mwa 46:2; Isa 41:10; Zab 58:11; 84:11; Ebr 11:6 Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.

2Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski?

3Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.

4 Mwa 17:16; 2 Sam 7:12 Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali utakayemzaa ndiye atakayekurithi.

5Rum 4:18; Ebr 11:12; Zab 147:4; Kut 32:13 Akamtoa nje, akasema, Tazama juu mbinguni kisha uzihesabu nyota, kama unaweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.

6Rum 4:3-6,20-25; Zab 106:31; Gal 3:6; Yak 2:23 Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.

7Mdo 7:2 Kisha akamwambia, Mimi ni BWANA, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uimiliki.

8 Amu 6:36-40; 1 Sam 14:9,10; 2 Fal 20:8; Lk 1:18 Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitaimiliki?

9Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo dume wa miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa.

10Akampatia hao wote, akawapasua vipande viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua.

11Na tai walipotua juu ya mizoga Abramu akawafukuza.

12Ayu 4:13,14; Mwa 2:21 Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia.

13Kut 1:1-14; 12:40; Mdo 7:6 BWANA akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa kwa muda wa miaka mia nne.

14Kut 6:6; 7:14; Kut 12:40-41; Mdo 7:7 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali nyingi.

15Mwa 25:8; Ayu 5:26; Ebr 11:13 Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.

16Mt 23:32; 1 The 2:16; 2 Pet 3:8,9 Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana uovu wa Waamori haujatimia bado.

17Ikawa, jua lilipokuchwa likawa giza, tazama, tanuri ya moshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vile vipande vya nyama.

18 Mdo 7:5; Mwa 17:8; Kum 1:7; Hes 34:3; 2 Nya 9:26; Neh 9:8; Zab 105:11 Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,

19Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni,

20na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai,

21na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, na Myebusi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help