Isaya 47 - Swahili Revised Union Version DC

Kuaibishwa kwa Babeli

1 Yer 48:18; Omb 2:3,10; Isa 13:1—14:23; Yer 50:1—51:64 Haya, shuka, keti mavumbini,

Ewe bikira, binti Babeli;

Keti chini pasipo kiti cha enzi,

Ewe binti wa Wakaldayo;

Maana hutaitwa tena mwororo, mpenda anasa.

2 Kut 11:5 Twaa mawe ya kusagia, usage unga;

Vua utaji wako, ondoa mavazi yako,

Funua mguu wako, pita katika mito ya maji.

3 Nah 3:5; Mt 7:2; Rum 12:19 Uchi wako utafunuliwa,

Naam, aibu yako itaonekana.

Nitalipa kisasi; simkubali mtu yeyote.

4Mkombozi wetu, BWANA wa majeshi ndilo jina lake,

Mtakatifu wa Israeli.

5 1 Sam 2:9; Dan 2:37 Kaa kimya, ingia gizani,

Ee binti wa Wakaldayo;

Maana hutaitwa tena Malkia wa falme.

6 2 Nya 28:9; Isa 10:6; Zek 1:15; Kum 28:50 Nilikuwa nimekasirika na watu wangu, niliutia unajisi urithi wangu, nikawatia mkononi mwako; wewe hukuwatendea rehema; kwa wazee uliifanya nira yako kuwa nzito sana.

7Ufu 18:7 Ukasema, Mimi nitakuwa malkia milele; hata hukuyatia hayo moyoni mwako, wala hukukumbuka mwisho wa mambo hayo.

8 Sef 2:15; Ufu 18:7-8 Sasa, basi, sikia haya, wewe upendaye anasa, ukaaye na kujiona salama, wewe usemaye moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi; sitaketi kama mjane, wala sitajua kufiwa na watoto;

91 The 5:3; Dan 2:2; Nah 3:4; 2 The 2:9,10; Ufu 9:21 lakini mambo haya mawili yatakupata katika dakika moja siku moja, kufiwa na watoto, na ujane; yatakupata kiasi kamili, uchawi wako ujapokuwa mwingi, na uganga wako mwingi mno.

10Zab 52:7; Eze 8:12 Maana umeutumainia ubaya wako; umesema, Hapana anionaye; hekima yako, na maarifa yako yamekupotosha, nawe umesema moyoni mwako, Mimi ndiye, wala hapana mwingine zaidi yangu mimi.

11Isa 13:6; Dan 5:30; Lk 17:27 Kwa sababu hiyo uovu utakupata; wala hutaweza kuuagua; na msiba utakuangukia; hutaweza kuuondoa; na ukiwa usioujua utakupata kwa ghafla.

12Simama sasa na uganga wako, na wingi wa uchawi wako, uliojitaabisha nao tangu ujana wako; labda utaweza kupata faida, labda utaweza kushinda.

13Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wanajimu, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe kutoka kwa mambo yatakayokupata.

14Nah 1:10; Mal 4:1 Tazama, watakuwa kama mabua makavu; moto utawateketeza; hawatajiokoa kutoka kwa nguvu za muali wa moto; hili halitakuwa kaa la kujipasha moto, wala moto wa kuota.

15Ufu 18:11 Ndivyo yatakavyokuwa mambo hayo uliyojitaabisha nayo; wale waliofanya biashara nawe tangu ujana wako watatangatanga mbali nawe, kila mtu akienda zake; hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help