Isaya 26 - Swahili Revised Union Version DC

Wimbo wa Yuda wa ushindi

1Siku ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda;

Sisi tunao mji ulio na nguvu;

Ataamuru wokovu kuwa kuta na maboma.

2 Zab 118:19; Isa 60:11; Ufu 21:13,24-27 Fungueni malango yake,

Taifa lenye haki, lishikalo kweli, liingie.

3Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea

Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.

4Mtumainini BWANA siku zote

Maana BWANA YEHOVA ni mwamba wa milele.

5Kwa kuwa amewashusha wakaao juu,

Mji ule ulioinuka, aushusha,

Aushusha hadi chini, auleta hadi mavumbini.

6Mguu utaukanyaga chini,

Naam, miguu yao walio maskini,

Na hatua zao walio wahitaji.

7 Kum 32:4 Njia yake mwenye haki ni unyofu;

Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki.

8 Zab 18:22; Isa 64:5; Mal 4:4; Lk 1:6 Naam, katika njia ya hukumu zako

Sisi tumekungoja, Ee BWANA;

Shauku ya nafsi zetu inaelekea

Jina lako na ukumbusho wako.

9 Zab 63:6; 83:16; Wim 3:1; Lk 6:12 Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku;

Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema;

Maana hukumu zako zikiwapo duniani,

Watu wakaao duniani hujifunza haki.

10 Mhu 8:12; Rum 2:4; Zab 143:10 Mtu mbaya ajapofadhiliwa,

Hata hivyo hatajifunza haki;

Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu,

Wala hatauona utukufu wa BWANA.

11 Ayu 34:27; Ebr 10:27 BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.

12BWANA, utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote.

13Zab 66:12 Ee BWANA, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.

14Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.

15Umeliongeza hilo taifa, BWANA, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.

16 2 Nya 33:12; Hos 5:15 BWANA, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.

17Kama vile mwanamke mwenye mimba anayekaribia wakati wake wa kuzaa, alivyo na uchungu na kulia kwa sababu ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa sisi mbele zako, Ee BWANA.

18Zab 17:14 Tumekuwa na mimba, tumekuwa na uchungu, tumekuwa kana kwamba tumezaa upepo; hatukufanya wokovu wowote duniani, wala hawakuanguka wakaao duniani.

19Isa 25:8; Hos 13:14; Yn 5:28,29; Dan 12:2 Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.

20 Mwa 7:1; Zab 30:5; 2 Kor 4:17 Njooni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita.

21Mik 1:3; Yud 1:14 Kwa maana, tazama, BWANA anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help