Zaburi 52 - Swahili Revised Union Version DC

Hukumu kwa waongoKwa mwimbishaji. Utenzi wa Daudi, wakati Doegi, Mwedomu alipomwendea Sauli na kumwambia, “Daudi ameingia nyumbani mwa Ahimeleki.”

1 1 Sam 22:9-10; 21:7 Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari?

Wema wa Mungu upo sikuzote.

2 Zab 50:19; Mit 12:18; Zab 59:7 Ulimi wako watunga madhara,

Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila.

3 Yer 9:4 Umependa mabaya kuliko mema,

Na uongo kuliko kusema kweli.

4Umependa maneno yote ya kupoteza watu,

Ewe ulimi wenye hila.

5 Mit 2:22 Lakini Mungu atakuharibu hata milele;

Atakuondolea mbali;

Atakunyakua hemani mwako;

Atakung'oa katika nchi ya walio hai.

6 Ayu 22:19; Zab 58:10 Nao wenye haki wataona;

Wataingiwa na hofu na kumcheka;

7 Ayu 31:24,25; Zab 49:6 Kumbe! Huyu ndiye mtu yule,

Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake.

Aliutumainia wingi wa mali zake,

Na kufanya mali kimbilio lake.

8 Zab 92:13 Bali mimi ni kama mzeituni

Umeao katika nyumba ya Mungu.

Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.

9 Zab 54:6 Nitakushukuru milele kwa maana umetenda;

Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema;

Mbele ya wacha Mungu wako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help