Zaburi 57 - Swahili Revised Union Version DC

Sifa na hakikisho katika matesoKwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Usiharibu. Utenzi wa Daudi alipomponyoka Sauli na kujificha pangoni.

1 Isa 26:20 Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi,

Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe.

Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako,

Hadi misiba hii itakapopita.

2 Zab 138:8 Nitamwita MUNGU Aliye Juu,

Mungu anitimiziaye mambo yangu.

3 Zab 144:5; 40:11 Atanitumia msaada toka mbinguni na kuniokoa,

Atawaaibisha wale wanaotaka kunishambulia.

Mungu atazituma

Fadhili zake na kweli yake.

4 Mit 30:14; Zab 64:3 Nafsi yangu i kati ya simba,

Nitastarehe kati yao waliowaka moto.

Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale,

Na ndimi zao ni upanga mkali.

5 Zab 108:5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,

Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.

6 Zab 9:15 Wameweka wavu ili kuninasa miguu;

Nimevunjika moyo;

Wamechimba shimo njiani mwangu;

Lakini wao wenyewe wametumbukia humo!

7 Zab 108:1 Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti,

Moyo wangu ni thabiti.

Nitaimba, nitaimba kwa sauti nzuri,

8 Amu 5:12 Amka, ee moyo wangu.

Amka, kinanda na kinubi,

Nitaamka alfajiri.

9Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu,

Nitakuimbia sifa kati ya mataifa.

10 Zab 108:4 Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,

Na uaminifu wako hata mawinguni.

11Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,

Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help