Mambo ya Walawi 24 - Swahili Revised Union Version DC

Taa isiyozimika

1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

2Kut 27:20; 39:37; Hes 8:2-4 Waagize wana wa Israeli wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya ile nuru, ili hiyo taa iwake daima.

3Hapo nje ya pazia la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeneza tangu jioni hadi asubuhi mbele za BWANA daima; ni amri ya milele katika vizazi vyenu.

4Kut 31:8; 37:17-24 Atazitengeneza hizo taa katika kile kinara kilicho safi mbele za BWANA daima.

Mikate ya Hema Takatifu

5 Kut 25:30; 40:24 Nawe utatwaa unga mwembamba, na kuoka mikate kumi na miwili ya huo unga; sehemu za kumi mbili za efa, zitakuwa katika mkate mmoja.

61 Fal 7:48; 2 Nya 4:19; Ebr 9:2 Nawe iweke mistari miwili, mikate sita kwa kila mstari, juu ya hiyo meza safi, mbele za BWANA.

7Nawe utatia ubani safi juu ya kila mstari, ili uwe ukumbusho kwa hiyo mikate, sadaka ya kusongezwa kwa BWANA kwa moto.

8Hes 4:7; 1 Nya 9:32; 2 Nya 2:4 Kila siku ya Sabato ataipanga mbele za BWANA daima; ni kwa ajili ya wana wa Israeli, agano la milele.

9Mt 12:4; Mk 2:26; Lk 6:4; 1 Sam 21:6; Kut 29:33; Law 8:3; 21:22 Nayo itakuwa ya Haruni na wanawe; nao wataila katika mahali patakatifu; kwa sababu kwake ni takatifu sana katika sadaka zitolewazo kwa BWANA kwa moto, kwa amri ya milele.

Kufuru na adhabu yake

10Ikawa mwanamume mmoja ambaye mama yake ni Mwisraeli, na babaye ni Mmisri, alitokea kati ya wana wa Israeli akalikufuru; na kupigana na Mwisraeli katika kambi;

11Ayu 1:5; 2:5,9; Isa 8:21; Kut 18:22 kisha huyo mwanamume ambaye mama ni Mwisraeli akakufuru jina la Bwana na kulaani nao watu wakampeleka kwa Musa. Mama yake mtu huyo alikuwa akiitwa Shelomithi, binti ya Dibri, wa kabila la Dani.

12Hes 15:34; Kut 18:15,16 Nao wakamtia kifungoni, ili wapate kuambiwa neno litakalotoka kinywani pa BWANA.

13Na BWANA akasema na Musa, na kumwambia,

14Kum 17:7 Mtoe huyo aliyelaani nje ya kambi; na wale wote waliomsikia na waweke mikono yao kichwani mwake, kisha mkutano wote na wamwue kwa kumpiga kwa mawe.

15Law 5:1; 9:13 Nawe nena na wana wa Israeli na kuwaambia, Mtu yeyote atakayemlaani Mungu wake atachukua dhambi yake.

161 Fal 21:10; Zab 74:10,18; Mt 12:31; Mk 3:28; Yak 2:7 Na yeyote atakayelaani jina la BWANA hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzaliwa, hapo atakapolaani jina la BWANA atauawa.

17Kut 21:12; Mwa 9:6; Hes 35:31; Kum 19:11; Mt 26:52; Ufu 13:10 Na mtu ampigaye mtu hadi akafa, lazima atauawa;

18na atakayempiga mnyama hadi akafa atalipa; uhai kwa uhai.

19Kut 21:24; Kum 19:21; Mt 5:38; 7:2 Na mtu akimtia mwenziwe kilema; vile vile kama alivyofanya, naye atafanyiwa vivyo hivyo;

20Kut 21:23-25; Kum 19:21; Mt 5:38 jeraha kwa jeraha, jicho kwa jicho, jino kwa jino; vile vile kama alivyomtia mtu kilema, naye atalipwa vivyo hivyo.

21Kut 21:33 Na mtu amwuaye mnyama atalipa; na yeye atakayemwua binadamu atauawa.

22Hes 15:16; Kut 12:49; Law 19:34; Kum 10:17,19 Mtakuwa na sheria moja tu, kwa huyo aliye mgeni, na kwa mzalia; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.

23Kum 13:9; 17:7 Musa akanena na wana wa Israeli, nao wakamtoa huyo aliyeapiza nje ya kambi, wakamwua kwa kumpiga kwa mawe. Wana wa Israeli wakafanya kama BWANA alivyomwagiza Musa.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help