1 nitaubomoa mnara huu.
10 Amu 7:12; 2 Fal 3:26 Basi hao kina Zebu na Salmuna walikuwa katika Karkori, na majeshi yao walikuwa pamoja nao, watu kama elfu kumi na tano hesabu yao, ni wote waliobaki wa hilo jeshi lote la hao wana wa mashariki; kwa sababu walianguka wapiganaji elfu mia moja na ishirini waliokuwa wakitumia upanga.
11Hes 32:35; Amu 18:27; Mit 17:18; 1 The 5:3 Basi Gideoni alikwea kwa njia iliyotumiwa na misafara, ambayo ilikuwa mashariki mwa Noba na Yogbeha, akalishambulia hilo jeshi; kwa maana lile jeshi halikuwa na hadhari.
12Zab 83:11 Zeba na Salmuna walikimbia; naye akawaandamia; akawakamata hao wafalme wawili wa Midiani Zeba na Salmuna, akalitapanyatapanya hilo jeshi lote.
13Kisha huyo Gideoni mwana wa Yoashi akarudi kutoka vitani, kutoka kwenye makweleo ya Heresi.
14Ndipo akamshika kijana mmoja mwanamume katika watu wa Sukothi, akamwuliza; naye akamwandikia majina ya hao wakuu wa Sukothi, na wazee wa mji, watu sabini na saba.
15Kisha akaufikia wale watu wa Sukothi, akawaambia, Tazama, Zeba na Salmuna, ambao ninyi mlinisimanga kwa ajili yao, mliposema, Je! Mikono ya Zeba na Salmuna iko sasa mikononi mwako wewe, hata tuwape watu wako waliochoka mikate?
16Basi akawatwaa hao wazee wa mji, na miiba ya nyikani na michongoma, akawafunza hao watu wa Sukothi kwayo.
171 Fal 12:25 Kisha akaubomoa mnara wa Penieli, na kuwaua watu wa mji huo.
18Amu 4:6; Zab 89:12 Ndipo akawaambia hao Zeba na Salmuna, Hao watu mliowaua huko Tabori walikuwa watu wa namna gani? Wakamjibu, Walikuwa kama wewe ulivyo; kila mmoja alikuwa anafanana na wana wa mfalme.
19Naye akasema, Watu hao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu; kama yeye BWANA aishivyo, kama mngaliwaokoa hai watu hao, nami nisingewaua ninyi.
20Kisha akamwambia Yetheri mwanawe mzaliwa wa kwanza, Haya, simama, uwaue hawa. Lakini huyo kijana hakutoa upanga wake; maana, akaogopa, kwa sababu alikuwa ni kijana tu.
21Zab 83:11 Ndipo hapo Zeba na Salmuna wakasema, Simama wewe utuue sisi; kwa maana kama mtu alivyo, ndivyo zilivyo nguvu zake. Basi Gideoni akasimama, akawaua Zeba na Salmuna, akazitwaa koja zilizokuwa katika shingo za ngamia wao.
Gideoni aabudu sanamu22Ndipo watu wa Israeli wakamwambia Gideoni, Tawala wewe juu yetu, wewe, na mwanao, na mjukuu wako pia; kwa kuwa wewe umetuokoa na mikono ya Midiani.
231 Sam 8:7; 10:19; Zab 10:16; 29:10; Isa 26:13; 33:22; Hos 13:10 Gideoni akawaambia, Mimi sitatawala juu yenu wala mwanangu hatatawala juu yenu; yeye BWANA atatawala juu yenu.
24Mwa 16:10; 25:13 Kisha Gideoni akawaambia, Mimi nina haja yangu niitakayo kwenu, ni ya kila mtu kunipa hizo herini za mateka wake. (Kwa maana walikuwa na herini za dhahabu, kwa sababu walikuwa ni Waishmaeli.)
25Wakajibu, Tutakupa kwa moyo mweupe. Basi wakatandika nguo chini, wakatia humo kila mtu herini za mateka yake.
26Na uzani wa hizo herini za dhahabu alizozitaka ulipata shekeli za dhahabu elfu moja na mia saba; mbali na makoja na vidani, na mavazi ya rangi ya zambarau waliyokuwa wameyavaa hao wafalme wa Midiani, tena mbali na mikufu iliyokuwa katika shingo za ngamia wao.
27Amu 17:5; 18:14,17; 6:24; Kut 23:33; Zab 73:27; 106:39; Kum 7:16 Basi Gideoni akafanya naivera kwa vitu vile, akaiweka katika mji wake, mji huo wa Ofra; nao Israeli wote wakaenda na kuiandama kwa ukahaba huko; nayo ilikuwa ni tanzi kwa Gideoni na kwa nyumba yake.
28Ndipo Midiani walishindwa mbele ya wana wa Israeli, wala hawakuinua vichwa vyao tena. Nayo nchi ilipata kuwa na amani muda wa miaka arubaini katika siku za Gideoni.
Kifo cha Gideoni29Kisha huyo Yerubaali, mwana wa Yoashi, akaenda kukaa katika nyumba yake mwenyewe.
30Amu 9:2,5; 10:4; 12:9,14 Gideoni alikuwa na wana sabini waliozawa na mwili wake; kwa maana alikuwa na wake wengi.
31Na suria yake aliyekuwako Shekemu, yeye naye akamzalia mwana, naye akamwita jina lake Abimeleki.
32Amu 6:24 Basi Gideoni mwana wa Yoashi akafa mwenye umri wa uzee mwema, akazikwa katika kaburi la Yoashi baba yake, katika Ofra ya Waabiezeri.
33 Amu 2:19; 9:4 Kisha ikawa, mara alipokufa Gideoni, wana wa Israeli wakakengeuka tena, wakawaandama Mabaali kwa ukahaba, wakamfanya Baal-berithi kuwa ni mungu wao.
34Zab 78:11,42; 106:13-21; Mhu 12:1; Yer 2:32 Kwani wana wa Israeli hawakumkumbuka BWANA, Mungu wao, ambaye ndiye aliyewaokoa na mikono ya adui zao wote pande zote;
35Amu 9:16; Mhu 9:14,15 wala hawakuifanyia mema nyumba ya Yerubaali, yaani Gideoni, licha ya hayo mema yote aliyowafanyia Waisraeli.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.