1 Ayu 13:6 Lakini, Ayubu, nakuomba usikilize hoja yangu,
Ukayasikilize maneno yangu yote.
2Tazama basi, nimefunua kinywa changu,
Ulimi wangu umenena kinywani mwangu.
3 1 The 1:3 Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu;
Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu.
4 Mwa 2:7 Roho ya Mungu imeniumba,
Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.
5Ikiwa unaweza, nijibu;
Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame.
6 Ayu 9:32 Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe;
Mimi nami nilifinyangwa katika udongo.
7 Ayu 13:21 Tazama, utisho wangu hautakutia hofu wewe,
Wala sitakulemea kwa uzito.
8Hakika umenena masikioni mwangu,
Nami nimesikia sauti ya maneno yako, ukisema,
9 Ayu 10:7 Mimi ni safi, sina makosa;
Sina hatia, wala hapana uovu ndani yangu;
10 Ayu 13:24 Tazama, yuaona sababu za kufarakana nami,
Hunihesabu kuwa ni adui yake;
11 Ayu 13:27 Hunitia miguu yangu katika mkatale,
Na mapito yangu yote huyapeleleza.
12 Mhu 7:20 Tazama, nitakujibu, katika neno hili huna haki;
Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.
13 Isa 45:9 Kwa nini unapingana naye, ukisema,
Hatajibu hata neno langu moja?
14Kwa kuwa Mungu hunena mara moja,
Naam, hata mara ya pili, ijapokuwa mtu hatambui.
15 Ayu 4:13 Katika ndoto, katika maono ya usiku,
Usingizi mzito uwajiapo watu,
Katika usingizi kitandani;
16Ndipo huyafunua masikio ya watu,
Na kuyatia mhuri mafundisho yao,
17Ili amwondoe mtu katika makusudio yake,
Na kumfichia mtu kiburi;
18Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni,
Na uhai wake usiangamie kwa upanga.
19 Kum 8:5; Zab 94:12,13 Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake,
Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;
20Hata roho yake huchukia chakula,
Na nafsi yake huchukia nyama nzuri.
21 Zab 102:5 Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane;
Na mifupa yake isiyoonekana yatokeza nje.
22Naam, nafsi yake inakaribia shimoni,
Na uhai wake unakaribia waangamizi.
23 2 Nya 36:15,16; Mal 2:7 Lakini akiwapo malaika pamoja naye,
Mpatanishi, mmoja katika elfu,
Ili kumwonesha binadamu hayo yampasayo;
24 Rum 3:24 Ndipo amwoneapo rehema, na kusema,
Mwokoe asishuke shimoni;
Mimi nimeuona ukombozi.
25Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto;
Huzirudia siku za ujana wake;
26 2 Fal 20:2-5; Zab 6:1-9 Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia;
Hata auone uso wake kwa furaha;
Naye humrejeshea mtu haki yake.
27Yeye huimba mbele ya watu, na kusema,
Mimi nimefanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea,
Wala sikulipizwa jambo hilo;
28Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni,
Na uhai wangu utautazama mwanga.
29Tazama, hayo yote ni Mungu anayeyafanya,
Mara mbili, naam, hata mara tatu, kwa mtu,
30 Zab 40:2; Zek 9:11 Ili kurudisha roho yake itoke shimoni,
Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai.
31Angalia sana, Ee Ayubu, unisikilize;
Nyamaza, mimi nitasema.
32 2 Kor 1:24 Kama una neno la kusema, nijibu;
Nena, kwani nataka kukuhesabia kuwa na haki.
33 Zab 34:11 Kama sivyo, unisikilize mimi;
Nyamaza, nami nitakufunza hekima.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.