2 Mambo ya Nyakati 23 - Swahili Revised Union Version DC

1 wakamtawaza kuwa mfalme; Yehoyada na wanawe wakamtia mafuta, wakasema, Mfalme na aishi.

Athalia auawa

12Na Athalia alipoisikia sauti ya watu, na ya walinzi, na ya hao waliomsifu mfalme, akaingia kwa watu nyumbani mwa BWANA;

131 Nya 25:8; 1 Fal 18:17,18; Rum 2:3 akatazama, na angalia, mfalme amesimama karibu na nguzo yake mlangoni, nao makamanda na wenye parapanda karibu na mfalme; wakafurahi watu wote wa nchi, wakapiga parapanda; waimbaji pia wakipiga vinanda, wakaongoza nyimbo za kusifu. Ndipo Athalia akararua mavazi yake, akasema, Uhaini! Uhaini!

14Hes 5:2; 19:14 Yehoyada kuhani akawaleta nje makamanda wa mamia, waliowekwa kuongoza jeshi, akawaambia, Mtoeni nje kati ya safu; na yeyote amfuataye, na auawe kwa upanga; kwani kuhani amesema, Msimwue katika nyumba ya BWANA.

15Neh 3:28; Mwa 9:5; 2 Nya 22:10; Mt 7:2 Basi wakampisha njia; akaenda kwa kuingia pa mlango wa farasi nyumbani mwa mfalme; nao wakamwua huko.

16 Kum 5:2,3; 2 Fal 11:17; 2 Nya 15:12; 29:10; Ezr 10:3; Neh 9:38 Kisha, Yehoyada akafanya agano, yeye na watu wote, na mfalme, kwamba watakuwa watu wa BWANA.

172 Fal 10:23; 11:18; 18:4; 2 Nya 34:4-7; Kum 13:9 Na watu wote wakaiendea nyumba ya Baali, wakaibomoa; wakavunjavunja madhabahu zake na sanamu zake, wakamwua Matani kuhani wa Baali mbele ya madhabahu.

181 Nya 23:6,30,31; 24:1; 25:2,6; Kut 29:38; Hes 28:2 Yehoyada akauamuru usimamizi wa nyumba ya BWANA chini ya mkono wa makuhani Walawi, aliowagawa Daudi nyumbani mwa BWANA, ili wazisongeze sadaka za kuteketezwa za BWANA, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, kwa kufurahi na kuimba, kama alivyoamuru Daudi.

191 Nya 26:1 Akawaweka walinzi malangoni pa nyumba ya BWANA, asiingie aliye najisi kwa namna yoyote.

202 Fal 11:19 Akawatwaa makamanda wa mamia, na watu wakubwa, na hao watawalao watu, na watu wote wa nchi, akamteremsha mfalme kutoka nyumba ya BWANA; wakalipitia lango la juu waende nyumbani kwa mfalme, wakamketisha mfalme katika kiti cha ufalme.

211 Sam 11:15; 1 Fal 1:40; 2 Fal 11:20; Zab 58:10; Mit 11:10; 29:2 Basi wakafurahi watu wote wa nchi, na mji ukatulia baada ya Athalia kuuawa kwa upanga.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help