Isaya 20 - Swahili Revised Union Version DC

Isaya aigiza kushindwa kwa Misri na Kushi

1 yule alipofika Ashdodi, alipotumwa na Sargoni mfalme wa Ashuru; naye alipigana na Ashdodi akautwaa;

2Zek 13:4; 1 Sam 19:24 wakati huo BWANA alinena kwa kinywa cha Isaya, mwana wa Amozi, akisema, Haya, uvue nguo ya magunia viunoni mwako, na viatu vyako miguuni mwako.

3Isa 8:18 Naye akafanya hivyo akaenda uchi, miguu yake ikiwa haina viatu. BWANA akasema, Kama vile mtumishi wangu Isaya anavyokwenda uchi, bila viatu, awe ishara na ajabu kwa muda wa miaka mitatu juu ya Misri na juu ya Kushi;

42 Sam 10:4; Mik 1:11 vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawachukua uchi, wafungwa wa Misri, na watu wa Kushi waliohamishwa, watoto kwa wazee, bila viatu, matako yao wazi, Misri iaibishwe.

52 Fal 18:21; Isa 31:1-3 Nao watafadhaika, na kuona haya kwa ajili ya Kushi, matumaini yao, na Misri, utukufu wao.

6Na mwenyeji wa nchi ya pwani atasema katika siku hiyo, Angalia, haya ndiyo yaliyowapata watu wale tuliowatumainia, ambao tuliwakimbilia watuokoe kutoka kwa mfalme wa Ashuru; na sisi je! Twawezaje kupona?

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help