1 ili amsaidie.
17Law 26:18 Kwa kuwa Waedomi walikuwa wamekuja tena, na kuwapiga Yuda, na kuwachukua wafungwa.
18Yos 15:22; Eze 16:27,57 Wafilisti pia walikuwa wameishambulia na kuitwaa miji ya Shemeshi, Ayaloni, Gederothi, soko, pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake na Gimzo pia na vijiji vyake, miji yake; wakakaa humo.
192 Nya 21:2; Kut 32:25; Ufu 3:17; 16:15 Kwa maana BWANA aliinamisha Yuda kwa ajili ya Ahazi mfalme wa Israeli; kwa kuwa yeye aliwafanyia Yuda aibu, na kumwasi BWANA mno.
202 Fal 15:29; 16:7-9; Isa 7:20 Na Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru akamjia, akamfadhaisha, asimtie nguvu kwa lolote.
21Kwa maana Ahazi alitwaa sehemu katika nyumba ya BWANA, na katika nyumba ya mfalme, na ya wakuu, akampa mfalme wa Ashuru; asisaidiwe na jambo hilo.
Ukaidi na kifo cha Ahazi22 2 Nya 33:12; Zab 50:15; Isa 1:5; Yer 5:3; Hos 5:15; Ufu 16:11 Na wakati alipofadhaishwa, akazidi kumwasi BWANA, huyo mfalme Ahazi.
232 Nya 25:14; Yer 44:17,18 Maana aliitolea dhabihu miungu ya Dameski iliyompiga, akasema, Kwa sababu miungu ya wafalme wa Shamu imewasaidia wao, mimi nitaitolea dhabihu, ili inisaidie mimi. Lakini ndiyo iliyomwangamiza yeye na Israeli wote.
242 Nya 29:3,7 Tena Ahazi akakusanya vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, akavikata vipande vipande vyombo vya nyumba ya Mungu, akaifunga milango ya nyumba ya BWANA; akajijengea madhabahu katika kila pembe ya Yerusalemu.
25Na katika kila mji wa Yuda akafanya mahali pa juu pa kuifukizia miungu mingine uvumba, akamkasirisha BWANA, Mungu wa babaze.
262 Fal 16:19,20; 2 Nya 20:34; 27:7-9 Basi mambo yake yote yaliyosalia, na njia zake zote, za kwanza hadi za mwisho, tazama, yameandikwa katika Kitabu cha Wafalme wa Yuda na Israeli.
27Ahazi akalala na babaze, wakamzika mjini, yaani, Yerusalemu; maana hawakumleta makaburini mwa wafalme wa Israeli; na Hezekia mwanawe akatawala mahali pake.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.