1 Rum 7:23; 1 Pet 2:11 Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?
2Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!
3Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
4Lk 6:26; Rum 8:7; 1 Yoh 2:15 Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.
5Kut 20:3,5; Mt 6:24; Gal 5:17 Au mwadhani ya kwamba Maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?
6Mit 3:34; Ayu 22:29; Mt 23:12; 1 Pet 5:5 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
7Efe 6:12; 1 Pet 5:8,9 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
8Zek 1:3; Isa 1:16 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
9Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni kubwa.
101 Pet 5:6 Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
Onyo juu ya kumhukumu mwingine11Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.
12Mk 7:1; Rum 2:1; 14:4 Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine?
Kujivuna juu ya kesho13 Mit 27:1 Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida;
14Lk 12:20; Zab 39:5,11 lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka.
15Mdo 18:21 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.
16Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya.
17Lk 12:47; Rum 14:23 Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.