Zaburi 75 - Swahili Revised Union Version DC

Shukrani kwa wema aliotenda MunguKwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Usiharibu. Zaburi ya Asafu. Wimbo.

1Ee Mungu, tunakushukuru.

Tunakushukuru kwa kuwa Jina lako liko karibu;

Watu huyasimulia matendo yako ya ajabu.

2Nitakapoufikia wakati ulioamriwa,

Mimi nitahukumu hukumu za haki.

3 Ebr 1:3 Ingawa dunia na wote wakaao humo wataharuki,

Mimi mwenyewe nimezisimamisha nguzo zake.

4Niliwaambia waliojivuna, Msijivune;

Na wasio haki, Msiiinue pembe.

5Msiiinue pembe yenu juu,

Wala msinene kwa shingo ya kiburi.

6Maana siko mashariki wala magharibi,

Wala nyikani itokako heshima.

7 1 Sam 2:7; 2 Sam 5:2; Dan 2:21; Lk 1:52 Bali Mungu ndiye ahukumuye;

Humdhili huyu na kumwinua huyu.

8 Ayu 21:20; Yer 25:15; Ufu 14:10 Maana mkononi mwa BWANA mna kikombe,

Na mvinyo yake inatoka povu;

Kumejaa machanganyiko;

Naye huyamimina.

Na sira zake wasio haki wa dunia

Watazifyonza na kuzinywa.

9Bali mimi nitatangaza matendo yako milele,

Nitamwimbia Mungu wa Yakobo.

10Nguvu zote za wasio haki nitazimaliza,

Lakini nguvu za mwenye haki nitaziimarisha.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help