Zaburi 32 - Swahili Revised Union Version DC

Shangwe kwa kusamehewaYa Daudi. Funzo

1 Rum 4:7-8; Zab 85:2 Heri aliyesamehewa dhambi,

Na kuondolewa makosa yake.

2 Law 17:4; Rum 5:13; Yn 1:47; 2 Kor 1:12 Heri ambaye BWANA hamhesabii hatia,

Na ambaye rohoni mwake hamna hila.

3Nilipokosa kuungama dhambi zangu, mifupa yangu ilipooza

Kwa kulia kwangu mchana kutwa.

4Kwa maana mchana na usiku

Mkono wako ulinilemea.

Jasho langu likakauka hata nikawa

Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.

5 Mit 28:13; Isa 65:24; Lk 15:18 Ndipo nikakuungamia dhambi yangu,

Wala sikuuficha upotovu wangu.

Nilisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA,

Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.

6 1 Tim 1:16; Isa 55:6; Yn 7:34 Kwa hiyo, hebu kila akuaminiye

Akuombe awapo katika dhiki.

Hakika maji makuu yafurikapo,

Hayatamfikia yeye.

7 Zab 9:9; Mit 18:10; Isa 4:6; Mt 23:37; Kol 3:3 Kimbilio langu utanilinda nisipate mateso,

Utanizungusha nyimbo za kufurahia wokovu wangu.

8 Isa 48:17 Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea;

Nitakushauri, jicho langu likikutazama.

9Msiwe kama farasi wala nyumbu,

Wasiokuwa na akili.

Kwa matandiko ya lijamu na hatamu

Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia.

10 Mit 13:21; Zab 34:8; Mit 16:20; Yer 17:7 Naye mtu mwovu ana mapigo mengi,

Bali amtumainiaye BWANA fadhili zitamzunguka.

11Mfurahieni BWANA;

Shangilieni, enyi wenye haki

Pigeni vigelegele vya furaha;

Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help