Waamuzi 9 - Swahili Revised Union Version DC

Abimeleki awania ufalme

1 chako sasa kiko wapi, hata ukasema, Huyo Abimeleki ni nani, hata inatupasa kumtumikia yeye? Je! Hawa sio majeshi hao uliowadharau wewe? Haya, toka nje sasa, tafadhali, upigane nao.

39Basi Gaali akatokeza mbele ya watu wa Shekemu, akapigana na Abimeleki.

40Lakini Abimeleki akamkimbiza, naye akakimbia mbele yake, wengi walijeruhiwa na kuanguka hadi kufikia maingilio ya lango la mji.

41Abimeleki akakaa Aruma; naye Zebuli akawatoa Gaali na ndugu zake, wasikae katika Shekemu.

42Ikawa siku ya pili yake, watu wakatoka waende mashambani; naye Abimeleki alipoambiwa.

43Akawatwaa watu wake, na kuwagawanya katika vikosi vitatu, nao wakavizia mashambani; naye akaangalia, alipoona watu wakitoka nje ya mji, aliwashambulia na kuwaua.

44Abimeleki, na vile vikosi vilivyokuwa pamoja naye, wakafululiza, wakasimama penye maingilio ya lango la mji, na vile vikosi viwili vikawarukia hao wote waliokuwa mashambani, na kuwaua.

45Kum 29:23; 1 Fal 12:25; 2 Fal 3:25; Ayu 8:22; Zab 9:16; 11:6; Mit 2:22; Mhu 8:12,13 Abimeleki akapigana na huo mji mchana kutwa; akautwaa mji, akawaua watu waliokuwamo ndani yake; kisha akauteketeza mji, na kuutia chumvi.

46 Amu 8:33; 1 Fal 18:26; 2 Fal 1:2-4; Zab 115:8; Isa 28:15-18 Kisha watu wote waliokaa katika ule mnara wa Shekemu waliposikia habari hiyo wakaingia ndani ya ngome ya nyumba ya El-berithi.

47Abimeleki aliambiwa ya kuwa watu hao wote wa mnara wa Shekemu wamekusanyika pamoja.

48Zab 68:14 Basi Abimeleki akakwea kwenda katika kilima cha Salmoni, yeye na wote waliokuwa pamoja naye; naye Abimeleki akashika shoka mkononi mwake, akakata tawi moja katika miti, akalishika na kujitwika begani mwake; akawaambia hao watu waliokuwa pamoja naye, “Haya, kile mlichoona nikifanya, nanyi fanyeni vivyo hivyo haraka”.

49Basi watu hao wote wakakata kila mtu tawi lake, wakamfuata Abimeleki, wakayaweka hayo matawi pale ngomeni, na kuiteketeza moto hiyo ngome juu yao; ndipo watu wote wa huo mnara wa Shekemu wakafa, watu wapatao elfu moja, wanaume kwa wanawake.

50 Kut 14:4; 2 Fal 14:10 Ndipo Abimeleki alipokwenda Thebesi, akauzingira na kuutwaa.

51Lakini ndani ya huo mji palikuwa na mnara wenye nguvu, na watu wote wanaume na wanawake wakakimbilia huko, na watu wote wa mji, nao wakajifungia ndani, wakapanda paa la mnara.

52Abimeleki akauendea huo mnara na kupigana nao; naye akaukaribia mlango wa mnara ili auteketeze.

532 Sam 11:21; Amu 4:17; Ayu 31:3; Yer 49:20; 50:45; 1 Kor 1:27 Na mwanamke mmoja akabwaga jiwe la kusagia la juu, nalo likampiga Abimeleki kichwani, na kulivunja fuvu la kichwa chake.

541 Sam 31:4 Ndipo akamwita kwa haraka huyo kijana aliyekuwa anamchukulia silaha zake, na kumwambia, Futa upanga wako, uniue, ili watu wasiseme juu yangu, Aliuawa na mwanamke. Basi huyo kijana wake akamchoma upanga, naye akafa.

55Basi hapo watu wa Israeli walipoona ya kuwa Abimeleki amekufa, wakaondoka wakaenda kila mtu mahali pake.

56Mwa 9:5,6; Ayu 31:3; Zab 9:12; 11:6; Mit 5:22; 24:12; Mdo 28:4; Rum 2:6; Gal 6:7; Ufu 19:20,21 Kwa hiyo, Mungu akalipiza kisasi juu ya uovu wa Abimeleki aliomtenda baba yake, kwa kuwaua hao nduguze watu sabini;

57uovu wote wa watu wa Shekemu Mungu alilipiza juu ya vichwa vyao; na hiyo laana ya Yothamu mwana wa Yerubaali ikawajia juu yao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help