1
45Lk 22:67 Nami, kwa sababu nasema iliyo kweli, hamnisadiki.
462 Kor 5:21; 1 Pet 2:22 Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?
47Yn 18:37; 1 Yoh 4:6 Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.
48 Yn 7:20; Mk 3:21 Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo?
49Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini mimi namheshimu Baba yangu, na ninyi mwanivunjia heshima yangu.
50Yn 5:41 Wala mimi siutafuti utukufu wangu; kuna yule autafutaye na ndiye hakimu.
51Yn 5:24; 6:40,47; 11:25 Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele.
52Mk 9:1 Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng'amua ya kuwa una pepo. Abrahamu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.
53Yn 4:12 Wewe u mkuu kuliko baba yetu Abrahamu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani?
54Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu; anitukuzaye ni Baba yangu, ambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu.
55Yn 7:28 Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nilishika.
56Abrahamu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.
57Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Abrahamu?
58Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Kabla ya Abrahamu kuwako, mimi niko.
59Yn 10:31 Basi wakaokota mawe ili wamtupie; lakini Yesu akajificha, akatoka hekaluni.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.