Estk A - Swahili Revised Union Version DC

UTANGULIZINdoto ya Mordekai

1a Njama juu ya mfalme

1l Basi, Mordekai alikuwa akipumzika behewani, kama kawaida yake, pamoja na Gabatha na Thara, matowashi wawili wa mfalme waliokuwa walinzi wa behewa.

1m Akasikia mazungumzo yao, akayapeleleza mashauri yao, akapata kufahamu ya kuwa wamejiweka tayari kumshika mfalme Artashasta. Akamwarifu mfalme habari zao.

1n Mfalme akawahoji wale matowashi wawili, nao wakakiri, wakapelekwa kuuawa.

1o Mfalme akayaandikisha mambo hayo kuwa ukumbusho, naye Mordekai pia aliandika habari zake.

1p Mfalme akamwagiza Mordekai atumike behewani, akamtunukia kwa kazi zake.

1q Ikawa Hamani mwana wa Hamedatha, Mbugaya, mtu mwenye heshima kuu kwa mfalme alikuwa ikiwatafuta mabaya Mordekai na watu wake kwa sababu ya hao matowashi wawili wa mfalme.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help