1 na moyo wake Farao ukawa mgumu asiwasikize; vile vile kama BWANA alivyonena.
Baa la nne: Inzi20 kati ya watu wangu na watu wako; ishara hiyo italetwa kesho.
24Zab 78:45 BWANA akafanya; wakaja inzi wengi kwa uzito sana, wakaingia nyumbani mwa Farao, na katika nyumba za watumishi wake, tena katika nchi yote ya Misri; nayo nchi iliharibiwa na wale inzi.
25Farao akawaita Musa na Haruni akawaambia, Endeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu ndani ya nchi hii.
26Musa akasema, Haitupasi kufanya hivyo; kwa kuwa tutamchinjia sadaka BWANA, Mungu wetu, na hayo machukizo ya Wamisri; je! Tutachinja sadaka ya hayo machukizo ya Wamisri mbele ya macho yao, wasitupige kwa mawe?
27Kut 3:12,18 La, tutakwenda safari ya siku tatu jangwani, tumchinjie dhabihu BWANA, Mungu wetu, kama atakavyotuagiza.
28Kut 9:28; 1 Fal 13:6; Ezr 6:10; Mdo 8:24 Farao akasema, Mimi nitawapa ruhusa mwende, ili mmchinjie dhabihu BWANA, Mungu wenu, jangwani; lakini hamtakwenda mbali sana; haya niombeeni.
29Musa akasema, Tazama, mimi natoka kwako, nami nitamwomba BWANA ili hao inzi wamtoke Farao, na watumishi wake, na watu wake kesho; lakini Farao asitende kwa udanganyifu tena, kwa kutowaacha watu waende kumchinjia BWANA dhabihu.
30Musa akatoka kwa Farao, akamwomba BWANA.
31Yak 5:17 BWANA akafanya kama neno la Musa, akawaondoa wale inzi wabaya kwake Farao, na kwa watumishi wake, na watu wake; hakusalia hata mmoja.
32Kut 4:21; Mit 28:14; Rum 9:17-23; Yak 1:13-17 Farao akaufanya moyo wake kuwa mzito mara hiyo nayo, wala hakuwapa ruhusa hao watu waende zao.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.