1 mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.
14Rum 12:2; Efe 2:3; 4:17 Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu;
15bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
16Law 11:44-45; 19:2; 20:7 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
17Zab 89:26; Yer 3:19; Mal 1:6; Mt 6:9; Rum 2:11 Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, nendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.
18Isa 52:3; 1 Kor 6:20; 7:23 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;
19Isa 53:7; Ebr 9:14 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na dosari wala waa, yaani, ya Kristo.
20Rum 16:25; Efe 1:4 Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa siku hizi za mwisho kwa ajili yenu;
21Yn 14:6; Rum 4:24; Kol 1:27 na kupitia kwake mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.
221 Yoh 5:1 Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo safi.
23Dan 6:26; Yn 1:13; Yak 1:18 Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, linalodumu hata milele.
24Isa 40:6-8; Yak 1:10,11 Maana,
Mwili wote ni kama majani,
Na fahari yake yote ni kama ua la majani.
Majani hukauka na ua lake huanguka;
25 Isa 40:8 Bali Neno la Bwana hudumu hata milele.
Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.