Isaya 10 - Swahili Revised Union Version DC

1Ole wao wawekao amri zisizo za haki, na waandishi waandikao sheria za kudhulumu;

2ili kumpotosha mhitaji asipate haki yake, na kuwanyang'anya maskini wa watu wangu haki yao; ili wajane wawe mateka yao, na kuwafanya yatima waliofiwa na baba zao kuwa mawindo yao!

3 matunda ya kiburi cha moyo wake mfalme wa Ashuru, na majivuno ya macho yake.

13Kut 15:9; Zab 20:7; Isa 37:24 Kwa maana amesema, Kwa nguvu za mkono wangu nimetenda jambo hili, na kwa hekima yangu; maana mimi nina busara; nami nimeiondoa mipaka ya watu, nikaziteka akiba zao, nikawaangusha waketio juu ya viti vya enzi kama afanyavyo shujaa.

14Na mkono wangu umezitoa mali za mataifa kama katika kiota cha ndege; na kama vile watu wakusanyavyo mayai yaliyoachwa, ndivyo nilivyokusanya dunia yote; wala hapana aliyetikisa bawa, wala kufumbua kinywa, wala kulia.

15Yer 51:20; Rum 9:20,21 Je! Shoka lijisifu juu yake alitumiaye? Je! Msumeno ujitukuze juu yake auvutaye? Ingekuwa kana kwamba bakora ingewatikisa waiinuao, au fimbo ingemwinua yeye ambaye si mti.

16Kwa hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, atatuma maradhi ya kukondesha kwa wapiganaji walionenepa; na badala ya utukufu wake kutawashwa kuteketea kama kuteketea kwa moto.

17Na mwanga wa Israeli utakuwa ni moto, na Mtakatifu wake atakuwa muali wa moto; nao utateketeza na kula mbigili zake na miiba yake kwa siku moja.

18Naye atauteketeza utukufu wa msitu wake, na wa shamba lake linalositawi, tangu nafsi hata nyama ya mwili, itakuwa kama vile afapo mtu aliye mgonjwa.

19Na miti ya msitu wake itakayosalia itakuwa michache, hata mtoto ataweza kuihesabu.

Mabaki ya Israeli waliotubu

20Tena itakuwa katika siku hiyo mabaki ya Israeli, na hao waliopona wa nyumba ya Yakobo, hawatamtegemea tena yeye aliyewapiga, bali watamtegemea BWANA, Mtakatifu wa Israeli, kwa kweli.

21Mabaki, nao ni mabaki ya Yakobo, watamrudia Mungu, aliye mwenye nguvu.

22Mik 5:3; Rum 9:27 Maana watu wako, Ee Israeli, wajapokuwa wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki tu watakaorudi; kuangamiza kumekusudiwa, kunakofurika kwa haki.

23Isa 28:22; Dan 9:27 Kwa maana Bwana, BWANA wa majeshi, atayatimiza maangamizo yaliyokusudiwa katika nchi yote.

24Kwa hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, asema hivi, Enyi watu wangu mkaao katika Sayuni, msiogope Ashuru, ingawa akupiga kwa fimbo, na kuliinua gongo lake juu yako, kama walivyofanya Wamisri.

25Dan 11:36 Maana bado kitambo kidogo tu ghadhabu itakoma, na hasira yangu itageukia kuwaangamiza.

26Na BWANA wa majeshi ataamsha mjeledi juu yake, kama vile alivyopiga Midiani karibu na jabali la Orebu; na fimbo yake itakuwa juu ya bahari, naye ataiinua kama walivyofanya Wamisri.

27Zab 105:15 Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.

28 Neh 11:31 Amefika Ayathi; amepita kati ya Migroni; ameweka mizigo yake huko Mikmashi;

291 Sam 13:23 wamevuka kivuko; wamekwenda kulala katika Geba; Rama unatetemeka; Gibea wa Sauli umekimbia.

301 Sam 25:44 Piga kelele sana, Ee binti Galimu; sikiliza, Ee Laisha; ole wako, maskini Anathothi!

31Yos 15:31 Madmena ni mkimbizi; wenyeji wa Gebimu wamejikusanya wakimbie;

321 Sam 21:1 siku hii ya leo atasimama huko Nobu; anatikisa mkono wake juu ya mlima wa binti Sayuni, mlima wa Yerusalemu.

33Angalia, Bwana, BWANA wa majeshi, atayakata matawi kwa nguvu za kutisha; nao walio warefu wa kimo watakatwa; na hao walioinuka wataangushwa chini;

34naye atavikata vichaka vya msitu kwa chuma; na Lebanoni utaanguka kwa mkono wake aliye mwenye uweza.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help