1Tazama, jicho langu limeyaona hayo yote,
Sikio langu limeyasikia na kuyaelewa.
2Hayo myajuayo ninyi, na mimi pia nayajua;
Mimi si duni kuliko ninyi.
3Hakika ningenena naye huyo Mwenyezi,
Nami nataka kuhojiana na Mungu.
4Lakini ninyi hubuni maneno ya uongo,
Ninyi nyote ni matabibu wasiofaa.
5
Ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake.
16 Isa 12:1,2 Hili nalo litakuwa ni wokovu wangu;
Kwani asiyemcha Mungu hatakaribia mbele yake.
17Sikieni sana maneno yangu,
Maelezo yangu na yaingie masikioni mwenu.
18Angalieni sasa, nimekwisha kulitengeneza neno langu,
Najua ya kuwa mimi ni mwenye haki.
19 Ayu 33:6; Isa 50:8 Yuko nani atakayeshindana nami?
Maana sasa nitanyamaza kimya na kukata roho.
Ayubu atoa ombi la kukata tamaa20Lakini msinifanyie mambo mawili, hayo tu,
Ndipo nami sitajificha usoni pako;
21Uondoe mkono wako usinilemee;
Na utisho wako usinitie hofu.
22Basi uite wakati huo, nami nitaitika;
Au, niache ninene mimi, nawe unijibu.
23Maovu yangu na dhambi zangu ni ngapi?
Nijulishe kosa langu na dhambi yangu.
24 Zab 10:1; Isa 8:17; Omb 2:5; 2 The 3:15 Mbona umeuficha uso wako,
Na kunihesabu kuwa ni adui yako?
25 Isa 17:13; 42:3 Je! Utalitaabisha jani lipeperushwalo?
Au, je! Utayafuatia hayo mabua makavu?
26 Zab 25:7 Kwani umeandika maneno ya uchungu juu yangu,
Na kunirithisha maovu ya ujana wangu;
27 Ayu 33:11 Waitia miguu yangu katika mkatale, na kuyakagua mapito yangu yote;
Wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu;
28Nijapokuwa ni kama kitu kilichooza, kinachosinyaa,
Mfano wa nguo iliyoliwa na nondo.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.