Zaburi 58 - Swahili Revised Union Version DC

Sala ya kutaka kisasiKwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Usiharibu. Utenzi wa Daudi.

1Ni kweli, enyi wakuu, mnanena haki?

Enyi wanadamu, mnahukumu kwa adili?

2 Zab 94:20 Sivyo! Mioyoni mwenu mnatenda maovu;

Mikono yenu wenyewe inaeneza udhalimu katika nchi.

3 Zab 51:5 Waovu hupotoka hata kabla ya kuzaliwa kwao;

Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.

4 Zab 140:4 Wana sumu mfano wa sumu ya nyoka;

Wao ni kama fira kiziwi azibaye sikio lake.

5Asiyeisikiliza sauti ya waganga,

Ijapo wanafanya uganga kwa ustadi.

6 Ayu 4:10 Ee Mungu, uyavunje meno yao vinywani mwao;

Ee BWANA, uyavunje magego ya wanasimba.

7Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi;

Akiielekeza mishale yake, iwe imetiwa ubutu.

8Kama konokono ayeyukaye na kutoweka,

Kama mimba iliyoharibika, isiyoliona jua,

9 Mit 10:25 Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba,

Ataipeperusha kama chamchela,

Iliyo mibichi na iliyo moto.

10 Kum 32:42; Ayu 22:19; Zab 18:47; Mit 10:11; Ufu 18:20 Mwenye haki atafurahi akionapo kisasi;

Ataiosha miguu yake katika damu ya wasio haki.

11 Rum 2:6-11; Ayu 34:11; Mhu 5:8; Yer 32:19; Eze 7:27; Rum 14:12; Ufu 2:23 Na mwanadamu atasema,

Hakika iko thawabu yake mwenye haki.

Hakika yuko Mungu

Anayehukumu katika dunia.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help