Ezra 8 - Swahili Revised Union Version DC

Wakuu wa koo walioandamana na Ezra

1Basi hawa ndio wakuu wa koo za baba zao, na hii ndiyo nasaba ya wale waliokwea pamoja nami kutoka Babeli, wakati wa kutawala kwake mfalme Artashasta.

2 mmoja wa wana wa Mali, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli; na Sherebia, pamoja na wanawe na ndugu zake, watu kumi na wanane;

19na Hashabia, na pamoja naye Yeshaya, wa wana wa Merari, na ndugu zake na wana wao, watu ishirini;

20Ezr 2:43 na katika Wanethini, ambao Daudi, na wakuu, walikuwa wamewaweka kwa ajili ya utumishi wa Walawi, Wanethini mia mbili na ishirini; wote wametajwa kwa majina yao.

Watu wafunga na kuomba amani

21 2 Nya 20:3; Law 16:29; Isa 58:3,5; Zab 5:8 Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote.

221 Kor 9:15; 1 Nya 28:9; Ezr 7:6,9; Zab 33:18,19; Isa 3:10; Rum 8:28; 1 Pet 3:12; Zab 34:16; 2 Nya 15:2 Maana niliona haya kumwomba mfalme kikosi cha askari na wapanda farasi, ili kutusaidia juu ya adui njiani; kwa maana tulikuwa tumesema na mfalme, tukinena, Mkono wa Mungu u juu ya watu wote wamtafutao, kuwatendea mema; bali uweza wake na ghadhabu yake ni juu ya wote wamkataao.

23Kum 4:29; 1 Nya 5:20; 2 Nya 33:13; Isa 19:22; Yer 29:12,13 Basi tukafunga, tukamsihi Mungu wetu kwa ajili ya hayo; naye akatutakabali.

Zawadi za hekaluni

24Ndipo nikawatenga watu kumi na wawili wa wakuu wa makuhani, nao ni Sherebia, na Hashabia, na watu kumi wa ndugu zao pamoja nao,

25Ezr 7:15,16 nami nikawapimia kwa mizani zile fedha, na dhahabu, na vile vyombo, matoleo kwa ajili ya nyumba ya Mungu wetu, ambayo mfalme, na washauri wake, na wakuu wake, na Waisraeli wote waliokuwapo, walikuwa wameyatoa;

26nami nikawapimia mikononi mwao talanta za fedha mia sita na hamsini na vyombo vya fedha talanta mia moja; na talanta mia moja za dhahabu;

27na mabakuli ishirini ya dhahabu, thamani yake darkoni elfu moja; na vyombo viwili vya shaba nzuri iliyong'aa, thamani yake sawa na dhahabu.

28Kum 33:8; Isa 52:11; Law 22:2,3; Hes 4:4; 1 Nya 23:28; 2 Nya 24:14 Kisha nikawaambia, Ninyi mmekuwa watakatifu kwa BWANA, na hivyo vyombo ni vitakatifu; na fedha na dhahabu ni matoleo ya hiari kwa BWANA, Mungu wa baba zenu.

291 Nya 26:20-26; Lk 12:37,38 Basi, angalieni, na kuvitunza vitu hivi, hata mtakapovipima mbele ya wakuu wa makuhani, na Walawi, na wakuu wa koo za mababa wa Israeli, huko Yerusalemu, katika vyumba vya nyumba ya BWANA.

30Hivyo makuhani na Walawi wakaupokea uzani wa fedha, na dhahabu, na vyombo, ili kuvileta Yerusalemu nyumbani kwa Mungu wetu.

Kurudi Yerusalemu

31 Ezr 7:6,9,28; Ayu 5:19-24; Isa 41:10-14 Ndipo tukasafiri toka mtoni Ahava siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza, ili kwenda Yerusalemu; na mkono wa Mungu ulikuwa pamoja nasi, akatuokoa na mkono wa adui, na mtu mwenye kutuvizia njiani.

32Neh 2:11 Tukafika Yerusalemu, tukakaa huko muda wa siku tatu.

33Hata siku ya nne, hizo fedha na dhahabu na vile vyombo vilipimwa ndani ya nyumba ya Mungu, vikatiwa mikononi mwa Meremothi, mwana wa Uria, kuhani; na pamoja naye alikuwapo Eleazari, mwana wa Finehasi; na pamoja nao Yozabadi, mwana wa Yeshua, na Noadia, mwana wa Binui, Walawi;

34vile vyombo vyote kwa hesabu na kwa uzani; tena uzani wake wote uliandikwa wakati ule.

35Ezr 6:17 Na wana wa uhamisho, waliokuwa wametoka katika uhamisho wakamtolea Mungu wa Israeli sadaka za kuteketezwa, ng'ombe kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, na kondoo dume tisini na sita, na wana-kondoo sabini na saba, na mabeberu kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi, hao wote pia walikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA.

36Ezr 7:21; Isa 56:6; 14:1; Zek 8:1-23 Wakawapa manaibu wa mfalme, na wakuu wa ng'ambo ya Mto, maagizo ya mfalme; nao wakawasaidia watu, na nyumba ya Mungu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help