Luka 19 - Swahili Revised Union Version DC

Yesu na Zakayo

1Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake.

2Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri.

3Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo.

4Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile.

5Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako.

6Akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha.

7Lk 15:2 Hata watu walipoona, walinung'unika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi.

8Kut 22:1; Hes 5:6,7 Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne.

9Lk 13:16; Mdo 3:25; 16:31 Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Abrahamu.

10Mt 18:11; Eze 34:16; Yn 3:17; Lk 5:32; 1 Tim 1:15 Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.

Mfano wa mafungu kumi ya fedha

11 Mt 25:14-30 Waliposikia hayo, aliongeza kusema mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu utaonekana mara moja. Lk 24:21; Mdo 1:6

12Mk 13:34 Basi akasema, Mtu mmoja, kabaila, alisafiri kwenda nchi ya mbali, ili ajipatie ufalme na kurudi.

13Akaita watu kumi katika watumwa wake, akawapa mafungu kumi ya fedha, akawaambia, Fanyeni biashara hadi nitakaporudi.

14Yn 1:11 Lakini watu wa mji wake walimchukia, wakatuma wajumbe kumfuata na kusema, Hatumtaki huyu atutawale.

15Ikawa aliporudi, ameupata ufalme wake, aliamuru waitwe wale watumwa aliowapa fedha, ili ajue faida aliyopata kila mtu kwa biashara yake.

16Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi.

17Lk 16:10 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.

18Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida.

19Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.

20Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka salama katika kitambaa.

21Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; wachukua usichoweka, wavuna usichopanda.

22Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, nichukuaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;

23basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake?

24Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang'anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi.

25Wakamwambia, Bwana, anayo mafungu kumi.

26Mt 13:12; Mk 4:25; Lk 8:18 Nawaambia, Kila aliye na kitu atapewa, bali yule asiye na kitu atanyang'anywa hata alicho nacho.

27Tena, wale adui zangu, wasiotaka niwatawale, waleteni hapa muwachinje mbele yangu.

Yesu aingia Yerusalemu kwa shangwe

28Na alipokwisha kusema hayo, alitangulia mbele akipanda kwenda Yerusalemu.

29 Mt 21:1-9; Mk 11:1-10; Yn 12:12-16 Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, kwenye mlima uitwao wa Mizeituni, alituma wawili katika wale wanafunzi,

30akisema, Nendeni mpaka katika kijiji kile kinachowakabili, na mtakapoingia ndani mtaona mwanapunda, amefungwa, ambaye hajapandwa na mtu yeyote bado, mfungueni mkamlete hapa.

31Na kama mtu akiwauliza, Mbona mnamfungua? Semeni hivi, Bwana anamhitaji.

32Na wale waliotumwa wakaenda wakaona kama alivyowaambia.

33Na walipokuwa wakimfungua mwanapunda, wenyewe waliwaambia, Mbona mnamfungua mwanapunda?

34Wakasema, Bwana anamhitaji.

35Wakampeleka kwa Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwanapunda, wakampandisha Yesu.

362 Fal 9:13 Na alipokuwa akienda walitandaza nguo zao njiani.

37Na alipokuwa amekaribia mteremko wa mlima wa Mizeituni, kundi zima la wanafunzi wake walianza kufurahi na kumsifu Mungu kwa sauti kuu, kwa ajili ya matendo yote ya uwezo waliyoyaona,

38Zab 118:26; Lk 2:14 wakasema, Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana; amani mbinguni, na utukufu huko juu.

39Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, uwakanye wanafunzi wako.

40Akajibu, akasema, Nawaambia ninyi, wakinyamaza hawa, mawe yatanena kwa sauti kuu.

Yesu aulilia Yerusalemu

41 2 Fal 8:11; Yn 11:35 Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia,

42Kum 32:29; Mt 13:14; Yn 12:38 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.

43Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;

44Lk 21:6; Zab 137:9 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiwa kwako.

Yesu atakasa hekalu

45 Mt 21:12-16; Mk 11:15-18; Yn 2:13-16 Akaingia hekaluni, akaanza kuwatoa wale waliokuwa wakifanya biashara,

46Isa 56:7; Yer 7:11 akiwaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.

47 Lk 21:37; 22:53; Yn 18:20 Naye akawa akifundisha kila siku hekaluni. Lakini wakuu wa makuhani, na waandishi, na wakuu wa watu walikuwa wakitafuta njia ya kumwangamiza;

48wasione la kutenda, kwa kuwa watu wote walikuwa wakiandamana naye, wakimsikiliza.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help