Ufunuo 9 - Swahili Revised Union Version

1 na kwa Kigiriki analo jina lake Apolioni.

12 Ufu 8:13; 11:14 Ole wao, pigo la kwanza limekwisha pita. Tazama, bado yako mapigo mawili, yanakuja baadaye.

13 Kut 30:1-3; Ufu 8:3 Malaika wa sita akapiga baragumu, nikasikia sauti moja iliyotoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyo mbele za Mungu,

14Mwa 15:18; Kum 1:7; Yos 1:4; Ufu 16:12 ikimwambia yule malaika wa sita aliyekuwa na baragumu, Wafungue nao malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Frati.

15Ufu 8:7-12 Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu.

16Na hesabu ya majeshi ya wapanda farasi ilikuwa milioni mia mbili; nilisikia hesabu yao.

17Hivyo ndivyo nilivyowaona hao farasi katika maono yangu, nao waliokaa juu yao, wana dirii kifuani, za wekundu kama wa moto, na buluu kama johari ya rangi ya samawati na manjano kama kiberiti, na vichwa vya farasi hao ni kama vichwa vya simba, na katika vinywa vyao hutoka moto na moshi na kiberiti.

18Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo matatu hayo, kwa moto huo na moshi huo na kiberiti hicho, yaliyotoka katika vinywa vyao.

19Kwa maana nguvu za hao farasi ni katika vinywa vyao, na katika mikia yao; maana mikia yao ni mfano wa nyoka, ina vichwa, nao wanadhuru kwavyo.

20Zab 115:4-7; 135:15-17; Dan 5:4,23; Isa 2:8,20; 17:8; 1 Kor 10:20; Ufu 16:9,11,21 Na wanadamu waliobakia, wasiouawa kwa mapigo hayo, hawakuzitubia zile kazi za mikono yao, hata wasiwasujudie mashetani, na sanamu za dhahabu na za fedha na za shaba na za mawe na za miti, zisizoweza kuona wala kusikia wala kutembea.

212 Fal 9:22 Wala hawakuutubia uuaji wao, wala uchawi wao, wala uasherati wao, wala wizi wao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help