2 Mambo ya Nyakati 12 - Swahili Revised Union Version

Wamisri waishambulia Yuda

1 2 Nya 11:17; Kum 8:14; 1 Fal 14:22-24 Ikawa ulipothibitika ufalme wa Rehoboamu, naye amepata nguvu, aliiacha Torati ya BWANA, na Israeli wote pamoja naye.

21 Fal 14:24,25 Ikawa katika mwaka wa tano wa mfalme Rehoboamu, akapanda Shishaki, mfalme wa Misri, juu ya Yerusalemu; kwa kuwa walikuwa wamemwasi BWANA;

32 Nya 16:8 akiwa na magari elfu moja na mia mbili, na wapanda farasi elfu sitini; na watu wasiohesabika, waliotoka Misri pamoja naye; Walubi, na Wasukii, na Wakushi.

4Akaitwaa miji yenye maboma iliyokuwa ya Yuda, akaja Yerusalemu.

52 Nya 11:2; Kum 28:25; 2 Nya 15:2 Ndipo akaja Shemaya nabii kwa Rehoboamu, na kwa wakuu wa Yuda, waliokusanyika Yerusalemu kwa sababu ya Shishaki, akawaambia, BWANA asema hivi, Ninyi mmeniacha mimi, kwa hiyo nami nimewaacha ninyi mkononi mwa Shishaki.

6Kut 10:3; Law 26:40-42; 2 Nya 33:12,19; 34:27; Zab 78:34; Yak 4:10; Kut 9:27 Ndipo wakajinyenyekeza wakuu wa Israeli na mfalme; wakasema, BWANA ndiye mwenye haki.

71 Fal 21:28,29 Naye BWANA alipoona ya kwamba wamejinyenyekeza, neno la BWANA likamjia Shemaya, kusema, Wamejinyenyekeza; sitawaharibu; lakini nitawapa wokovu punde, wala ghadhabu yangu haitamwagika juu ya Yerusalemu kwa mkono wa Shishaki.

8Isa 26:13; Kum 28:47,48 Walakini watamtumikia; ili wapate kujua utumwa wangu, na huo utumwa wa falme za nchi.

91 Fal 14:25,26; 10:16,17; 2 Nya 9:15,16 Basi Shishaki, mfalme wa Misri, akaushambulia Yerusalemu, akazichukua hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme; akazichukua zote. Akazichukua pia ngao za dhahabu alizozitengeneza Sulemani.

102 Sam 8:18; 23:23; 1 Nya 11:25 Mfalme Rehoboamu akafanya ngao za shaba mahali pake, akawakabidhi wakuu wa walinzi, waliongoja mlangoni pa nyumba ya mfalme.

11Ikawa kila wakati mfalme alipoingia nyumbani mwa BWANA, wakaja walinzi wakazichukua, wakazirudisha tena chumbani mwa walinzi.

12Mwa 18:24; 1 Fal 14:13; 2 Nya 19:3 Naye alipojinyenyekeza, ghadhabu ya BWANA ikamgeukia mbali, asimharibu kabisa; tena yalionekana katika Yuda mambo mema.

131 Fal 14:21; 2 Nya 13:7; 2 Nya 6:6; Zab 48:1-3 Basi mfalme Rehoboamu akajitia nguvu katika Yerusalemu, akatawala; maana Rehoboamu alikuwa na umri wa miaka arubaini na mmoja alipoanza kutawala, akatawala miaka kumi na saba huko Yerusalemu, mji aliouchagua BWANA miongoni mwa kabila zote za Israeli, ili aliweke huko jina lake. Na jina la mamaye aliitwa Naama Mwamoni.

14Mt 7:7; Mdo 9:11 Naye akatenda yaliyo maovu, kwa kuwa hakuukaza moyo wake amtafute BWANA.

152 Nya 9:29; 13:22 Basi mambo yake Rehoboamu, ya kwanza hadi za mwisho, je! Hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu Shemaya nabii na Ido mwonaji, kwa jinsi ya kuandika nasaba? Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu siku zote.

16Rehoboamu akalala na babaze, akazikwa katika mji wa Daudi. Na Abiya mwanawe alitawala mahali pake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help