1 Mambo ya Nyakati 4 - Swahili Revised Union Version

Wazawa wa Yuda

1

14 kwani hao walikuwa mafundi stadi.

15Na wana wa Kalebu, mwana wa Yefune; Iru, na Ela, na Naamu; na wana wa Ela; na Kenazi.

16Na wana wa Yehaleleli; Zifu, na Zifa, na Tiria, na Asareli.

17Na wana wa Ezrahi; Yetheri, na Meredi, na Eferi, na Yaloni; na Miriamu akamzalia na Shamai, na Ishba, babaye Eshtemoa.

18Na mkewe Myahudi akawazaa Yeredi, babaye Gedori, na Heberi, babaye Soko, na Yekuthieli, babaye Zanoa. Na hawa ndio wana wa Bithia, binti Farao, ambaye Meredi alimwoa.

19Na wana wa mkewe Hodia, dada yake Nahamu, walikuwa babaye Keila, Mgarmi, na Eshtemoa, Mmaaka.

20Na wana wa Shimoni; Amnoni, na Rina, na Ben-hanani, na Tiloni. Na wana wa Ishi; Zohethi, na Ben-zohethi.

21 Mwa 38:1 Wana wa Shela, mwana wa Yuda; Eri, babaye Leka, na Laada, babaye Maresha, na jamaa zao wa ukoo wa wafuma nguo za kitani safi, wa ukoo wa Ashbea;

222 Sam 8:2 na Yokimu, na watu wa Kozeba, na Yoashi, na Sarafi waliokuwa na mamlaka katika Moabu, na Yashubi-lehemu. (Na taarifa hizi ni za zamani sana).

23Hao ndio waliokuwa wafinyanzi, na wenyeji wa Netaimu na Gedera; ndipo walipokaa pamoja na mfalme ili kufanya kazi yake.

Wazawa wa Simeoni

24Wana wa Simeoni; Yemueli, na Yamini, na Yakini, na Sohari, na Shauli;

25na mwanawe huyo ni Shalumu, na mwanawe huyo ni Mibsamu, na mwanawe huyo ni Mishma.

26Na wana wa Mishma; mwanawe huyo ni Hamueli, na mwanawe huyo ni Zakuri, na mwanawe huyo ni Shimei.

27Naye Shimei alikuwa na wana wa kiume kumi na sita, na wana wa kike sita; lakini nduguze walikuwa hawana watoto wengi, tena jamaa yao yote haikuongezeka sana kama wana wa Yuda.

28Nao wakakaa huko Beer-sheba, na Molada, na Hasar-shuali;

29na huko Bilha, na Esemu, na Toladi;

30na huko Bethueli, na Horma, na Siklagi;

31na huko, Beth-markabothi, na Hasar-susimu, na Bethbiri, na Shaaraimu. Hiyo ndiyo miji yao hadi wakati wa kutawala kwa Daudi.

32Na vijiji vyao vilikuwa Etamu, na Aini, na Rimoni, na Tokeni, na Ashani, miji mitano,

33na vijiji vyote vilivyoizunguka miji iyo hiyo, mpaka Baali. Hayo ndiyo makao yao, na hati ya nasaba yao wanayo.

34Naye Meshobabu, na Yamleki, na Yosha, mwana wa Amazia;

35na Yoeli, na Yehu, mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli;

36na Elioenai, na Yaakoba, na Yeshohava, na Asaya, na Adieli, na Yesimieli, na Benaya;

37na Ziza, mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya;

38hao waliotajwa majina yao ndio waliokuwa wakuu katika jamaa zao; na koo za baba zao zikaongezeka sana.

39Basi wakaenda mpaka maingilio ya Gedori, naam, mpaka upande wa mashariki wa bonde hilo, ili kuwatafutia kondoo wao malisho.

40Mwa 9:22; 10:6; Zab 78:51 Wakaona malisho ya unono, mazuri, na nchi yenyewe ilikuwa wazi, tulivu na yenye amani; kwani waliokaa huko zamani walikuwa watu wa Hamu.

412 Fal 18:8 Na hao walioandikwa majina yao waliingia huko katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda, na kuziharibu hema zao, pamoja na hao Wameuni waliokuwa wakiishi huko, wakawaangamiza kabisa, hata siku hii ya leo, nao wakakaa huko badala yao; kwa sababu huko kulikuwa na malisho kwa kondoo wao.

42Na baadhi yao, wana wa Simeoni wapatao watu mia tano, wakaenda mpaka mlima Seiri, na majemadari wao walikuwa Pelatia, na Nearia, na Refaya, na Uzieli, wana wa Ishi.

431 Sam 15:8; 30:17; 2 Sam 8:12 Nao wakawaua Waamaleki waliokuwa wamenusurika, wakakaa huko, hata siku hii ya leo.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help