1 Zab 96:7-9; 1 Nya 16:28,29 Mpeni BWANA, enyi wana wa Mungu,
Mpeni BWANA utukufu na nguvu;
2Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;
Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu.
3Sauti ya BWANA inasikika juu ya maji;
Mungu wa utukufu apiga radi;
BWANA yu juu ya maji mengi.
4Sauti ya BWANA ina nguvu;
Sauti ya BWANA ina utukufu;
5Sauti ya BWANA yaivunja mierezi;
Naam, BWANA aivunjavunja mierezi ya Lebanoni;
6 Zab 114:4; Kum 3:9 Airusharusha Lebanoni kama ndama wa ng'ombe;
Lebanoni na Sirioni kama mwananyati.
7Sauti ya BWANA inatoa miale paa ya moto;
8 Hes 13:26 Sauti ya BWANA yalitetemesha jangwa;
BWANA alitetemesha jangwa la Kadeshi.
9Sauti ya BWANA yawazalisha ayala,
Na kuiacha misitu wazi;
Na ndani ya hekalu lake
Wanasema, Utukufu!
10 Zab 93:4 BWANA aketi juu ya Gharika;
Naam, BWANA ameshika hatamu ya ufalme milele.
11 Isa 40:29 BWANA na awape watu wake nguvu;
BWANA na awabariki watu wake kwa amani.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.