Zaburi 8 - Swahili Revised Union Version

Utukufu wa Mungu na hadhi ya utuKwa mwimbishaji: kwa kufuata Gitithi. Zaburi ya Daudi.

1Ee, MUNGU, Bwana wetu

Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!

Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;

2 Mt 21:16; 11:25; 1 Kor 1:27 Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao

Umeiweka misingi ya nguvu;

Kwa sababu yao wanaoshindana nawe;

Uwakomeshe adui na mjilipiza kisasi.

3 Zab 44:16; 19:1; Ayu 22:12; Rum 1:20 Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako,

Mwezi na nyota ulizoziratibisha;

4 Ayu 7:17-18; Zab 144:3; Ebr 2:6-8 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke,

Na binadamu hata umwangalie?

5Umemfanya mdogo kuliko Mungu;

Umemvika taji la utukufu na heshima;

6 1 Kor 15:27; Efe 1:22; Ebr 2:8; Mwa 1:26 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;

Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.

7Kondoo, na ng'ombe wote pia;

Naam, na wanyama wa porini;

8Ndege wa angani, na samaki wa baharini;

Na kila kipitacho njia za baharini.

9 Ayu 11:7; Zab 35:10 Wewe, MUNGU, Bwana wetu,

Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help