Zaburi 88 - Swahili Revised Union Version

Sala ya msaada katika wakati wa kukata tamaaWimbo. Zaburi ya Wakorahi. Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Mahalathi. Utenzi wa Hemani Mwezrahi.

1Ee BWANA, Mungu wa wokovu wangu

Mchana na usiku nimelia mbele zako.

2Maombi yangu yafike mbele zako,

Ukitegee kilio changu sikio lako.

3Maana nafsi yangu imeshiba taabu,

Na uhai wangu umekaribia kuzimu.

4Nimehesabiwa pamoja nao washukao shimoni;

Nimekuwa kama mtu asiye na msaada.

5Miongoni mwao waliokufa nimetupwa,

Kama waliouawa walalao makaburini.

Hao ambao Wewe huwakumbuki tena,

Wametengwa mbali na mkono wako.

6Mimi umenilaza chini katika shimo,

Katika mahali penye giza vilindini.

7Ghadhabu yako imenilemea,

Umenitesa kwa mawimbi yako yote.

8Wanijuao umewatenga nami;

Umenifanya kuwa chukizo kwao;

Nimefungwa wala siwezi kutoka.

9Jicho langu limefifia kwa ajili ya mateso

BWANA, ninakuita kila siku;

Ninakunyoshea Wewe mikono yangu.

10Je! Wafu utawafanyia miujiza?

Au waliofariki watasimama na kukuhimidi?

11Fadhili zako zitasimuliwa kaburini?

Au uaminifu wako katika uharibifu?

12 Ayu 10:21; Zab 31:12; Mhu 8:10 Miujiza yako itajulikana gizani?

Au haki yako katika nchi ya usahaulifu?

13Lakini mimi nimekulilia Wewe, BWANA,

Na asubuhi maombi yangu yatakuwasilia.

14BWANA, kwa nini kuitupa nafsi yangu,

Na kunificha uso wako?

15 Ayu 6:4; Isa 53:8; Dan 9:26 Nimeteswa tangu ujana wangu na niko karibu kufa,

Nimeumia kwa mapigo yako; nami nimekata tamaa.

16Hasira zako kali zimenizidia,

Mapigo yako yatishayo yameniangamiza.

17Yamenizunguka kama mafuriko mchana kutwa,

Yamenisonga kwa kila upande.

18 Ayu 19:13 Mpenzi na rafiki umewatenga nami,

Nao wanijuao wamo gizani.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help