Wafilipi 3 - Swahili Revised Union Version

1 Flp 2:18; 4:4 Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana.

Kuondokana na yaliyopita

Kuwaandikieni mambo yale yale hakuniudhi mimi, bali kutawafaa ninyi.

2 Ufu 22:15 Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao.

3Rum 2:29 Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili.

42 Kor 11:18,22 Lakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu yeyote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi.

5Mdo 23:6; 26:5; Rum 11:1; Lk 1:59; 2:21 Nilitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila la Benyamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo,

6Mdo 8:3; 22:4; 26:9-11 kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia.

7Mt 13:44,46 Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, niliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.

8Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;

9Rum 3:21,22 tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;

10Rum 6:3-5; 8:17; Gal 6:17 ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;

11Mdo 4:2; Ufu 20:5,6 ili nipate kwa njia yoyote kuufikia ufufuo wa wafu.

Kujitahidi kuelekea kwenye lengo

12 1 Tim 6:12; Mdo 9:6 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu.

13Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele;

141 Kor 9:24 nakaza mwendo, niifikie tuzo la thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.

151 Kor 2:6 Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hata mkiwaza mengine katika jambo lolote, Mungu atawafunulia hilo nalo.

16Gal 6:16 Lakini, hapo tulipofika na tuende katika lilo hilo.

17 1 Kor 4:16; 11:1; 1 The 1:7; 1 Pet 5:3 Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi.

181 Kor 1:23; Gal 6:12 Maana wengi huenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;

19Rum 16:18 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao uko katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.

20Efe 2:6; Kol 3:1; Ebr 12:22 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;

211 Kor 15:43,49,53 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help