Yoeli 1 - Swahili Revised Union Version

Maombolezo juu ya maangamizi ya nchi

1 Ebr 1:1; 2 Pet 1:21 Neno la BWANA lililomjia Yoeli, mwana wa Pethueli.

2 Kum 4:32; Isa 7:17; Dan 12:1; Yoe 2:2; Mt 24:21 Sikieni haya, enyi wazee;

Sikilizeni, enyi wenyeji wote wa nchi.

Je! Mambo haya yamekuwako katika siku zenu,

Au katika siku za baba zenu?

3 Zab 78:4 Waambieni watoto wenu habari yake,

Watoto wenu wakawaambie watoto wao,

Na watoto wao wakakiambie kizazi kingine.

4Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu.

5 Isa 32:10 Levukeni, enyi walevi, mkalie;

Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai;

Kwa sababu ya divai mpya;

Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu.

6 Mit 30:25; Ufu 9:8 Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu,

Lenye nguvu, tena halina hesabu;

Meno yake ni kama meno ya simba,

Naye ana magego ya simba mkubwa.

7 Isa 5:6 Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe.

8 Isa 22:12; Mit 2:17 Omboleza kama mwanamwali avaaye magunia

Kwa ajili ya mume wa ujana wake.

9 Yoe 2:14 Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji

Zimekatiliwa mbali na nyumba ya BWANA;

Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, wanaomboleza.

10 Yer 12:11; Isa 24:7 Shamba limeharibika, nchi inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka.

11 Yer 14:3 Tahayarini, enyi wakulima;

Pigeni yowe, enyi watunzaji wa mizabibu;

Kwa ajili ya ngano na shayiri,

Maana mavuno ya mashamba yamepotea.

12 Isa 9:3; Yer 48:33; Hos 9:1,2 Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia;

Nao mkomamanga na mtende na mtofaa;

Naam, miti yote ya mashamba imekauka;

Maana furaha imetoweka kwa wanadamu.

Mwito wa toba na sala

13 Yer 4:8 Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani;

Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu;

Njooni mlale usiku kucha katika magunia,

Enyi wahudumu wa Mungu wangu;

Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji

Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.

14 2 Nya 20:3,13 Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini,

Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi;

Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu,

Na kumlilia BWANA,

15 Yer 30:7; Yoe 2:3; Amo 5:16-18; Isa 13:6 Ole wake siku hii!

Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama maangamizi yatokayo kwake aliye Mwenyezi.

16Kum 12:7,12; 16:11 Je! Chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko mbali na nyumba ya Mungu wetu?

17Mbegu zinaoza chini ya udongo wake; mabohari yameachwa ukiwa; ghala zimeharibika; kwa maana nafaka imekauka.

181 Fal 18:5; Hos 4:3 Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng'ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana malisho; naam, makundi ya kondoo yamehangaika.

19Ee BWANA, nakulilia wewe;

Kwa maana moto umeyala malisho ya nyikani,

Na miali ya moto imeteketeza miti yote ya mashamba.

20 Ayu 38:41; Zab 104:31; 1 Fal 17:7 Naam, hata wanyama pori wanakulilia wewe;

Kwa maana vijito vya maji vimekauka,

Na moto umeyateketeza malisho ya nyikani.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help