Kumbukumbu la Torati 6 - Swahili Revised Union Version

Amri kuu

1Na hii ndiyo sheria, amri na hukumu, alizoziamuru BWANA, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayovuka kuimiliki;

2

5Mt 22:37; Mk 12:30-32; Lk 10:27; Kum 30:6; 1 Yoh 5:3 Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

6Kum 11:18-20; Isa 51:7 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;

7Efe 6:4 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyasema uishipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.

8Mit 6:21; Kut 13:9; Mit 3:3; 7:3 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.

9Kum 11:20; Isa 50:8; 57:8 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.

Hadhari ya kutotii

10 Mwa 12:7; 26:3; 28:13; Yos 24:13; Zab 105:44 Kisha BWANA Mungu wako atakapokuleta katika nchi aliyowaapia babu zako, Abrahamu na Isaka na Yakobo, ya kuwa atakupa; miji mikubwa mizuri usiyoijenga wewe,

11na nyumba zimejaa vitu vyema vyote usizojaza wewe, na visima vilivyochimbwa usivyochimba wewe, mashamba ya mizabibu na mizeituni usiyoipanda wewe, nawe utakula na kushiba;

12ndipo ujitunze, usije ukamsahau BWANA aliyekutoa nchi ya Misri, nyumba ya utumwa.

13Mt 4:10; Lk 4:8; Kum 13:4; Zab 63:11 Mche BWANA, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake.

14Yer 25:6 Msifuate miungu mingine katika miungu ya mataifa wawazungukao;

15kwani BWANA, Mungu wako, aliye katikati yako ni Mungu mwenye wivu; isije ikawaka juu yako hasira ya BWANA, Mungu wako, akakuangamiza kutoka juu ya uso wa nchi.

16 Kut 17:1-7; Mt 4:7; Lk 4:12; 1 Kor 10:9 Msimjaribu BWANA, Mungu wenu, kama mlivyomjaribu huko Masa.

17Zab 119:4 Zishikeni kwa bidii sheria za BWANA, Mungu wenu, na maagizo yake, na amri zake alizokuagiza.

18Nawe fanya yaliyo sawa, na mema, machoni pa BWANA; ili mpate kufanikiwa, nawe upate kuingia na kuimiliki nchi nzuri BWANA aliyowaapia baba zako,

19ya kuwa atawasukumia nje adui zako wote mbele yako, kama alivyosema BWANA.

20Na zamani zijazo atakapokuuliza mwanao, akikuambia, Ni nini mashuhudizo, na amri, na hukumu, alizowaagiza BWANA, Mungu wetu?

21Ndipo umwambie mwanao, Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri; BWANA, akatutoa kutoka Misri kwa mkono wa nguvu;

22BWANA akaonesha ishara na maajabu makubwa na mazito, juu ya Misri, Farao, na nyumba yake yote, mbele ya macho yetu;

23akatutoa huko ili kututia huku, apate kutupa nchi aliyowaapia babu zetu.

24Ayu 35:7,8; Yer 32:39; Zab 41:2; Lk 10:28 BWANA akatuamuru kuzifanya amri hizi zote, tumche BWANA, Mungu wetu, tuone mema sikuzote ili atuhifadhi hai kama hivi leo.

25Rum 10:3 Tena itakuwa haki kwetu, tukizingatia kufanya maagizo haya yote mbele ya BWANA, Mungu wetu, kama alivyotuagiza.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help