1Haleluya.
Msifuni Mungu katika patakatifu pake;
Msifuni katika anga la uweza wake.
2Msifuni kwa matendo yake makuu;
Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3Msifuni kwa mvumo wa baragumu;
Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4 Kut 15:20; Isa 38:20 Msifuni kwa matari na kucheza;
Msifuni kwa zeze na filimbi;
5Msifuni kwa matoazi yaliayo;
Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6 Ufu 5:13 Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA.
Haleluya.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.