1 Mt 5:48; Kol 3:12 Hivyo mwigeni Mungu, kama watoto wanaopendwa;
2Kut 29:18; Zab 40:6; Gal 2:20; Ebr 10:10; Kol 3:13; Eze 20:41 mkaende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.
Zikataeni njia za kipagani3 Efe 4:19; Kol 3:5 Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;
4Efe 4:29; Kol 3:8 wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali kuwepo kushukuru.
51 Kor 6:9,10; Kol 3:5; Mdo 8:21 Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, (ndiye mwabudu sanamu), aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.
6Rum 1:18; Kol 2:4,8 Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.
7Basi msishirikiane nao.
8Efe 2:11,13; Lk 16:8; 1 Pet 2:9; Yn 12:36 Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; nendeni kama watoto wa nuru,
9kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli;
10Rum 12:2 mkihakiki ni nini impendezayo Bwana.
11Yn 16:8 Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;
12Rum 1:24 kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena.
13Yn 3:20,21 Lakini chochote kinachoangazwa na nuru hudhihirishwa, maana chochote kile kilichoadhihirika ni nuru.
14Isa 26:19; 60:1; Rum 13:11; 6:13 Hivyo husema,
Amka, wewe usinziaye,
Ufufuke katika wafu,
Na Kristo atakuangaza.
15 Mt 10:16; Kol 4:5 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16Kol 4:5 mkiukomboa wakati kwa maana nyakati hizi ni za uovu.
17Rum 12:2 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
18Mit 23:31; Lk 21:34 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;
19Kol 3:16-17; Zab 33:2,3 mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;
20Kol 3:17 na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo.
Nyumba ya Kikristo21 1 Pet 5:5 Hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.
22 Kol 3:18; 1 Pet 3:1; Mwa 3:16 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.
231 Kor 11:3; Kol 1:18 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
24Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
25 Kol 3:19; 1 Pet 3:7 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
26Tit 3:5 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
27Zab 45:13; 2 Kor 11:2 apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na dosari wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
28Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
29Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea kanisa.
30Efe 1:23; 1 Kor 6:15; Mwa 2:23 Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake.
31Mwa 2:24 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
32Ufu 19:7 Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na kanisa.
33Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.