1 Wathesalonike UTANGULIZI - Swahili Revised Union Version

UTANGULIZIThesalonike ulikuwa mji mkuu wa mkoa wa Waroma wa Makedonia. Paulo alifika huko kutoka Filipi wakati wa ziara yake ya pili ya kueneza Injili (tazama Mdo 17:1-10), akakaa huko kwa miezi kadhaa. Lakini kutokana na chuki ya Wayahudi waliokuwa huko ilimbidi kuondoka na kwenda Berea (17:10).Waraka huu wa kwanza wa Paulo kwa Wathesalonike labda uliandikwa mnamo mwaka wa 50 B.K. Wengi wanafikiri kwamba miongoni mwa maandishi yote ya Agano Jipya, Waraka huu ni wa zamani kuliko mengine yote.Paulo anaanza kwa maneno ambayo yanaonesha kwamba jumuiya ya Wathesalonike ilikuwa jumuiya aliyoipenda sana kama mfano mzuri wa imani kwa Kristo. Mara nyingi Paulo katika sehemu ya kwanza ya waraka huu anagusia juu ya imani yao thabiti (1:3-10; 2:14). Anawaambia kwamba wao walipokea Injili kwa msaada wa Roho Mtakatifu na uthabiti mkubwa (1:5), wakawa mfano mzuri kwa Wakristo wengine (1:7). Anamshukuru Mungu kwa ajili ya habari nzuri alizopokea kutoka kwa Timotheo (3:1-6).Sehemu muhimu ya Waraka huu ni sura 4:11—5:11. Wakristo wa Thesalonike walikuwa wanaogopa itakavyokuwa wakati Yesu atakaporudi, hasa kwa kuwa jamaa zao waliomwamini Yesu walikuwa wamekwisha kufa. Paulo anawahakikishia kwamba Wakristo waliokwisha kufa watashiriki kikamilifu katika mema ya kuja kwake Kristo.
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help