Hesabu 14 - Swahili Revised Union Version

Watu wanaasi

1Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule.

2Ukaidi wa Waisraeli na kushindwa kwao

26Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,

27Kut 16:28; Mt 17:17; Mk 9:19; Kut 16:12; 1 Kor 10:10 Je! Nivumilie na mkutano mwovu huu uninung'unikiao hadi lini? Nimesikia manung'uniko ya wana wa Israeli, waninung'unikiayo.

28Ebr 3:17 Waambieni, Kama niishivyo, asema BWANA, hakika yangu kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi;

29Hes 26:64 mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi, hao walioninung'unikia,

30Kum 1:36,38 hakika yangu hamtaingia ninyi katika nchi, ambayo niliapa kwa kuinua mkono wangu, kwamba nitawafanyia makao humo, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.

31Zab 106:24; Mit 1:25,26; Ebr 12:16,17 Lakini Watoto wenu, ambao mlisema watakuwa mateka, ndio nitakaowaleta na kuwatia ndani, nao wataijua nchi mliyoikataa ninyi.

321 Kor 10:5 Lakini katika habari zenu, maiti zenu zitaanguka katika jangwa hili.

33Mdo 7:36; Zab 107:40; Kum 2:14 Kisha watoto wenu watakuwa wachungaji jangwani muda wa miaka arubaini nao watauchukua mzigo wa uasherati wenu, hadi maiti zenu zitakapoangamia jangwani.

34Hes 13:25; Zab 95:10; Eze 4:6; 1 Fal 8:56; Zab 77:8; Ebr 4:1 Kwa jumla ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arubaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arubaini, nanyi mtakujua kuchukizwa kwangu.

35Hes 23:19 Mimi BWANA nimekwisha nena, hakika yangu ndilo nitakaloutenda mkutano mwovu huu wote, waliokusanyika juu yangu; wataangamia katika nyika hii, nako ndiko watakakokufa.

36Hes 13:31 Kisha hao watu, ambao Musa aliwatuma waipeleleze nchi, waliorudi, na kufanya mkutano wote kumnung'unikia, kwa walivyoleta habari mbaya juu ya nchi,

37Yer 28:16,17; 1 Kor 10:10; Ebr 3:17; Yud 1:5 watu hao walioileta habari mbaya ya nchi wakafa kwa tauni mbele ya BWANA.

38Yos 14:6 Lakini Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, wakabaki hai miongoni mwa wale watu waliokwenda kuipeleleza nchi.

39 Mit 19:3; Mt 8:12; Ebr 12:17 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli wote maneno haya, na hao watu wakaomboleza sana.

40Kum 1:41; Mhu 9:3; Mt 7:21; Lk 13:25 Wakainuka na mapema asubuhi, wakakwea juu ya mlima hata kileleni, wakisema, Tazameni, sisi tupo hapa, nasi tutakwea kwenda mahali BWANA alipotuahidi; kwani tumefanya dhambi.

412 Nya 24:20; Ayu 9:4; Isa 59:1,2; Yer 2:37; 1 Kor 10:22 Musa akawaambia, Kwa nini ninyi sasa kuyakaidi maagizo ya BWANA? Maana halitafanikiwa jambo hilo.

42Kum 1:42; Zab 44:1-3 Msikwee, kwa kuwa BWANA hayumo kati yenu; msipigwe na kuangushwa mbele ya adui zenu.

43Kum 1:43,44; Amu 16:20 Kwa kuwa Mwamaleki na Mkanaani wako mbele yenu, nanyi mtaanguka kwa upanga, kwa sababu mmerudi nyuma msimfuate BWANA, kwa hiyo BWANA hatakuwa pamoja nanyi.

44Lakini walithubutu kukwea mlimani hata kileleni; ila sanduku la Agano la BWANA halikutoka humo kambini, wala Musa hakutoka.

45Ndipo Mwamaleki, na Mkanaani waliokaa huko mlimani, wakateremka, wakawapiga na kuwaangusha, hadi wakafika Horma.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help