Ayubu 17 - Swahili Revised Union Version

Ayubu aomba apate faraja

1 Zab 88:3,4 Roho yangu imezimia, siku zangu zimekoma,

Kaburi i tayari kunipokea.

2 1 Sam 1:6 Ni kweli wako kwangu wenye kufanya dhihaka,

Jicho langu hukaa katika kunifanyia uchungu kwao.

3 Mit 6:1 Nipe rehani basi, uwe dhamana kwa ajili yangu kwako wewe mwenyewe;

Kuna nani atakayeniwekea dhamana?

4Kwa kuwa umezifumba akili zao ufahamu;

Kwa hiyo hutawaacha wanishinde.

5Awafitiniye rafiki zake wawe mawindo,

Hata macho ya watoto wake yataingia kiwi.

6 1 Fal 9:7 Amenifanya niwe mithali kwa watu;

Nimekuwa mwenye kuchukiwa kwa wazi.

7Jicho langu nalo limekuwa giza kwa sababu ya majonzi,

Na viungo vyangu vyote vimekuwa kama kivuli.

8Walekevu watayastaajabia hayo,

Na asiye na hatia atajiamsha juu ya mpotovu.

9 Mit 4:18; Zab 24:4 Lakini mwenye haki ataishika njia yake,

Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu.

10 Ayu 6:29 Lakini rudini; ninyi nyote, njoni sasa;

Wala sitampata mtu mwenye hekima kati yenu.

11 Ayu 7:6; Isa 38:10 Siku zangu zimepita, makusudi yangu yamevunjika,

Hata hayo niliyo nayo moyoni mwangu.

12Wabadili usiku kuwa mchana;

Wasema, Mwanga u karibu kwa sababu ya giza.

13Nikitazamia kuzimu kuwa nyumba yangu;

Nikitandika malazi yangu gizani;

14Ikiwa nimeuita uharibifu, Wewe u baba yangu;

Na kuliambia buu, Wewe u mama yangu, na dada yangu;

15Basi, tumaini langu liko wapi?

Na tumaini langu, ni nani atakayeliona?

16 2 Kor 1:9; Zab 88:4-8; Ayu 3:17 Litashuka kwenye makomeo ya kuzimu,

Itakapokuwapo raha mavumbini.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help