Zaburi 56 - Swahili Revised Union Version

Kumtumaini Mungu katika matesoKwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Njiwa Mkimya wa Mbali. Utenzi wa Daudi alipokamatwa na Wafilisti kule Gathi.

1 Zab 31:9 Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza,

Mchana kutwa ananionea akileta vita.

2 Zab 57:3 Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa,

Maana ni wengi wanaonipiga vita.

3 1 Sam 30:6; 2 Nya 20:3 Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe;

4 Ebr 13:5,6 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.

Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;

Mwenye mwili atanitenda nini?

5Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu,

Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya.

6 Mdo 4:27,28 Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu,

Kwa kuwa waliniotea ili waniue.

7Je! Wataokoka kwa uovu wao?

Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako.

8 Mal 3:16 Umehesabu kutangatanga kwangu;

Uyatie machozi yangu katika chupa yako;

(Je! Hayamo katika kitabu chako?)

9 Isa 8:9,10 Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo.

Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;

10Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.

Kwa msaada wa BWANA nitalisifu neno lake.

11Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;

Mwanadamu atanitenda nini?

12 Zab 116:14-16 Ee Mungu, nadhiri zako ziko juu yangu;

Nitakutolea dhabihu za kushukuru.

13 Ayu 33:30 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti;

Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke?

Ili niende mbele za Mungu

Katika nuru ya walio hai.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help