Hesabu 20 - Swahili Revised Union Version

Maji ya Meriba

1 kwa sababu wana wa Israeli waliteta na BWANA, naye alijionesha kuwa mtakatifu kati yao.

Njia ya kupitia Edomu yakataliwa

14 Amu 11:16,17; Kum 23:7; Oba 1:10,12 Kisha Musa akatuma wajumbe kutoka Kadeshi wamwendee mfalme wa Edomu, na kusema, Ndugu yako Israeli asema, Wewe wazijua taabu zote zilizotupata;

15jinsi baba zetu walivyoteremkia Misri, nasi tulikaa Misri muda mrefu, nao Wamisri walitutenda vibaya sana, na baba zetu pia;

16Kut 2:23; 3:7; Mdo 7:35 tena tulipomlilia BWANA, akatusikiza sauti yetu, akamtuma malaika, na kututoa Misri; nasi tupo hapa Kadeshi, mji wa mpakani mwa nchi yako;

17Hes 21:22 tafadhali utupe ruhusa tupite katika nchi yako; hatutapita katika mashamba, wala katika mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visimani; tutaifuata njia kuu ya mfalme, tusigeuke kwenda upande wa kulia, wala upande wa kushoto, hadi tutakapotoka katika nchi yako.

18Edomu akamwambia, Hutapita katika nchi yangu, nisije nikakutokea kupigana nawe kwa upanga.

19Kum 2:6,28 Wana wa Israeli wakamwambia, Tutakwea kwa njia kuu; tena kama tukinywa maji yako, mimi na wanyama wangu wa mifugo, ndipo nitakulipa thamani yake; nipe ruhusa nipite kwa miguu yangu wala sitaki neno lingine lolote.

20Mwa 27:41; 32:6; Amu 11:17; Zab 120:7; Eze 35:5,11; Amo 1:11 Akamwambia, Hutapita katika nchi yangu. Kisha Edomu akamtokea ili kupigana naye, na watu wengi, na kwa mkono wa nguvu.

21Kum 2:27,29; Amu 11:18; Rum 12:18; Ebr 12:14 Basi hivyo Edomu akakataa kumpa Israeli ruhusa kupita katika mipaka yake; kwa hiyo Israeli akageuka na kumwacha.

Kifo cha Haruni

22 Hes 33:37; 21:4 Kisha wakasafiri kutoka Kadeshi; wana wa Israeli, mkutano mzima, wakafikia mlima wa Hori.

23BWANA akanena na Musa na Haruni katika mlima wa Hori, karibu na mpaka wa nchi ya Edomu, akawaambia,

24Mwa 25:8; Hes 27:13; Isa 57:1,2; Ebr 12:23 Haruni atakusanywa awe pamoja na watu wake; kwa kuwa hataingia katika nchi niliyowapa wana wa Israeli, kwa sababu mliasi kinyume cha neno langu hapo penye maji ya Meriba.

25Kum 32:50 Uwatwae Haruni na mwanawe Eleazari uwalete juu ya mlima wa Hori;

26umvue Haruni mavazi yake, ukamvike Eleazari mwanawe mavazi hayo; kisha Haruni atakusanywa kwa watu wake, naye atakufa huko.

27Musa akafanya kama BWANA alivyomwagiza; wakakwea katika mlima wa Hori mbele ya macho ya mkutano wote.

28Kut 29:29; Hes 33:38; Kum 10:6; Hes 23:10; Ayu 30:23; Mit 14:32; Hos 13:14; Ufu 14:13 Kisha Musa akamvua Haruni mavazi yake, akamvika mwanawe Eleazari mavazi hayo; Haruni akafa huko katika kilele cha mlima; Musa na Eleazari wakateremka mlimani.

29Mwa 50:3,10; Kum 34:8 Na mkutano wote ulipoona ya kuwa Haruni amekufa, wakamwombolezea Haruni muda wa siku thelathini, maana, nyumba yote ya Israeli ikamwombolezea.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help