Wimbo ulio Bora 8 - Swahili Revised Union Version

1Laiti ungekuwa kama ndugu yangu,

Aliyeyanyonya matiti ya mamangu!

Kama ningekukuta huko nje,

Ningekubusu, asinidharau mtu.

2

Ningekunywesha divai iliyokolea,

Divai mpya ya mkomamanga wangu.

3 Wim 2:6; Isa 62:4,5; 2 Kor 12:9 Mkono wake wa kushoto ungekuwa chini ya kichwa changu,

Nao wa kulia ungenikumbatia.

4Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,

Msiyachochee mapenzi, au kuyaamsha,

Hadi yatakapokuwa tayari.

Kurudi nyumbani

5 Yn 17:14 Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani,

Akimtegemea mpendwa wake?

Nilikuamsha chini ya huo mpera;

Huko mama yako alikuonea uchungu,

Aliona uchungu aliyekuzaa.

6 Isa 49:16; Yer 22:24; Hag 2:23; Flp 3:8 Nitie kama mhuri moyoni mwako,

Kama mhuri juu ya mkono wako;

Kwa maana upendo una nguvu kama mauti,

Na wivu ni mkali kama ahera.

Mwako wake ni mwako wa moto,

Na miali yake ni miali ya Yahu.

7 Mit 6:35 Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,

Wala mito haiwezi kuuzamisha;

Kama mtu angetoa badala ya upendo

Mali yote ya nyumbani mwake,

Angedharauliwa kabisa.

8 Zab 22:27 Kwetu sisi tuna dada mdogo,

Wala hana matiti;

Tumfanyieje dada yetu,

Siku atakapoposwa?

9 Ufu 3:20 Kama akiwa tu ukuta,

Tumjengee buruji za fedha;

Na kama akiwa ni mlango,

Tumhifadhi kwa mbao za mierezi.

10 Kol 2:7; Eze 16:7 Mimi nilikuwa ukuta,

Na matiti yangu kama minara;

Ndipo nikawa machoni pake

Kama mtu aliyeipata amani.

11 Mt 21:33 Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baal-hamomi

Akawakodisha walinzi hilo shamba lake la mizabibu;

Kila mtu atoe vipande elfu moja vya fedha kwa matunda yake.

12Shamba langu la mizabibu, lililo langu mimi, liko mbele yangu.

Basi, Sulemani, wewe uwe na elfu zako,

Na hao wayalindao matunda yake wapewe mia mbili.

13 Wim 2:14 Wewe ukaaye bustanini,

Hao rafiki huisikiliza sauti yako;

Unisikizishe mimi.

14 Wim 2:17 Ukimbie, mpendwa wangu,

Nawe uwe kama paa, au ayala,

Juu ya milima ya manukato.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help