1 na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kulelewa wa mfalme Herode, na Sauli.
2 nanyi mnaomcha Mungu, sikilizeni.
17Kut 1:7; 12:51; Isa 1:2; Kut 6:1,6; 12:37,41; 14:8 Mungu wa watu hawa Israeli aliwachagua baba zetu, akawatukuza watu hao, walipokuwa wakikaa kama wageni katika nchi ya Misri, na kwa mkono ulioinuliwa akawatoa, akawaongoza.
18Hes 14:34; Kum 1:31; Kut 16:35 Na kwa muda wa miaka kama arubaini akawavumilia katika jangwa.
19Kum 7:1; Yos 14:1 Na alipokwisha kuwaangamiza mataifa saba katika nchi ya Kanaani akawapa nchi yao iwe urithi kwa muda wa miaka kama mia nne na hamsini;
20Amu 2:16; 1 Sam 3:20 baada ya hayo akawapa waamuzi hata wakati wa nabii Samweli.
211 Sam 8:5; 10:21,24 Hatimaye wakaomba kupewa mfalme; Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila la Benyamini, kwa muda wa miaka arubaini.
221 Sam 13:14; 16:12,13; Zab 89:20; Isa 44:28; Ebr 1:5; 5:5 Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.
232 Sam 7:12; Isa 11:1 Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani, Yesu, kama alivyoahidi;
24Mk 1:4; Lk 3:3 Yohana alipokuwa amekwisha kuwahubiria watu wote wa Israeli habari za ubatizo wa toba, kabla ya kuja kwake.
25Mt 3:11; Mk 1:7; Lk 3:16; Yn 1:20,27 Naye Yohana alipokuwa akimaliza mwendo wake alinena, Mnadhani mimi ni nani? Mimi siye. Lakini, angalieni, anakuja mmoja nyuma yangu ambaye mimi sistahili kumlegezea viatu vya miguu yake.
26 Zab 107:20; Mdo 13:46 Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Abrahamu, na hao miongoni mwenu wanaomcha Mungu, kwetu sisi neno la wokovu huu limepelekwa.
27Mdo 3:17; Yn 16:3 Kwa maana wakaao Yerusalemu, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii yanayosomwa kila sabato, wameyatimiza kwa kumhukumu.
28Mt 27:22-23; Mk 15:13-14; Lk 23:21-23; Yn 19:15 Na ijapokuwa hawakuona sababu ya kumwua wakamwomba Pilato auawe.
29Mt 27:57-61; Mk 15:42-47; Lk 23:50-56; Yn 19:38-42 Hata walipokwisha kumaliza yote aliyoandikiwa, wakamteremsha kutoka kwa ule mti, wakamweka kaburini.
30Mdo 3:15 Lakini Mungu akamfufua katika wafu;
31Mdo 1:3 akaonekana siku nyingi na wale waliopanda naye kutoka Galilaya hadi Yerusalemu, ambao sasa ndio walio mashahidi wake mbele ya watu.
32Mdo 13:23 Na sisi tunawahubiria Habari Njema ya ahadi ile waliyopewa mababa,
33Zab 2:7 ya kwamba Mungu amewatimizia watoto wetu ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu; kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili,
Wewe ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa.
34 Isa 55:3 Tena ya kuwa alimfufua katika wafu, asipate kurudia uharibifu, amenena hivi,
Nitawapa ninyi mambo matakatifu ya Daudi yaliyo amini.
35 Zab 16:10; Mdo 2:27 Kwa hiyo anena na pengine,
Hutamwachia Mtakatifu wako kuona uharibifu.
36 1 Fal 2:10; Amu 2:10; Mdo 2:29 Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.
37Bali huyu aliyefufuliwa na Mungu hakuona uharibifu.
38 Mdo 10:43; Hes 15:30; Ebr 9:9; 13:20 Basi, na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi;
39Rum 10:4 na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa Torati ya Musa.
40Hab 1:5 Angalieni, basi, isiwajie habari ile iliyonenwa katika manabii.
41 Hab 1:5 Tazameni, enyi mnaodharau,
kastaajabuni, mkatoweke;
kwa kuwa natenda kazi mimi siku zenu,
kazi ambayo msingeisadiki kabisa,
ijapo mtu akiwasimulia sana.
42Na walipokuwa wakitoka, wakawasihi waambiwe maneno haya sabato ya pili.
43Mdo 11:23 Sinagogi ilipofumukana, Wayahudi na waongofu watauwa wengi wakawafuata Paulo na Barnaba; ambao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu.
44Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu.
45Mdo 13:50; 14:2 Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana.
46Mdo 3:26; 18:6; Mt 10:6; Lk 7:30 Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona ninyi wenyewe kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.
47Isa 42:6; 49:6 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana,
Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa,
Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.
48 Mdo 11:18; Rum 8:29 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini.
49Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote.
50Lakini Wayahudi wakawachochea wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao.
51Mt 10:14; Mk 6:11; Lk 9:5; 10:11; Mdo 18:6 Nao wakawakung'utia mavumbi ya miguu yao, wakaenda Ikonio.
52Lakini wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.