1 Wafalme 15 - Swahili Revised Union Version

Abijamu atawala Yuda: Kuabudu sanamu na vita

1Mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya alianza kutawala juu ya Yuda.

2 na Yeroboamu siku zote za maisha yake.

72 Nya 13:2,3,22 Na mambo yote ya Abiya yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda? Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.

82 Nya 14:1 Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi. Akatawala Asa mwanawe mahali pake.

Asa atawala Yuda

9Mwaka wa ishirini wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa alianza kutawala juu ya Yuda.

10Akatawala miaka arubaini na mmoja huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Maaka, binti Absalomu.

112 Nya 14:2; 15:17 Basi, Asa akafanya yaliyo mema machoni pa Mungu, kama alivyofanya babaye Daudi.

121 Fal 14:21; 22:46 Akawafukuza mahanithi katika nchi, akaziondoa sanamu zote walizozifanya baba zake.

13Kum 13:6; 33:9; 2 Nya 15:16; Mt 10:37; 19:29; Lk 12:51,53; 14:26; Kut 32:20 Hata na Maaka, mamaye, akamwondolea daraja yake asiwe malkia, kwa kuwa amefanya sanamu ya kuchukiza kwa Ashera; basi Asa akaikata sanamu yake akaiteketeza penye kijito cha Kidroni.

141 Fal 22:43; 2 Nya 15:17 Lakini mahali pa juu hapakuondoshwa; ila moyo wake Asa ulikuwa mkamilifu kwa BWANA siku zake zote.

15Akavileta vile vitu alivyovitakasa baba yake, na vile alivyovitakasa yeye mwenyewe, katika nyumba ya BWANA, fedha; na dhahabu, na vyombo.

Ushirikiano na Shamu juu ya Israeli

16Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli siku zao zote.

17 2 Nya 16:1; Yos 18:25; 1 Sam 15:34; 1 Fal 12:27 Kisha, Baasha mfalme wa Israeli akashambulia Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu yeyote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda.

181 Fal 20:1-5,33,34; 2 Fal 8:7-15; 2 Nya 16:2; Mwa 14:15; 1 Fal 11:23 Ndipo Asa akazitwaa fedha zote na dhahabu zilizosalia katika hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme, akazitia mikononi mwa watumishi wake; mfalme Asa akawatuma kwa Ben-hadadi, mwana wa Tabrimoni, mwana wa Hezioni, mfalme wa Shamu, aliyekaa Dameski, akasema,

19Tumepatana mimi nawe, na baba yangu na baba yako; angalia, nimekuletea zawadi, fedha na dhahabu; basi nenda, uyavunje mapatano yako na Baasha mfalme wa Israeli, ili aache mashambulizi juu yangu.

202 Fal 15:29; Amu 18:29; 2 Sam 20:14 Naye Ben-hadadi akamsikiliza mfalme Asa, akawatuma wakuu wa majeshi yake juu ya miji ya Israeli, akapiga Iyoni, na Dani, na Abel-beth-maaka na Kinerothi yote, na nchi yote ya Naftali.

21Ikawa Baasha aliposikia habari hiyo akaacha kuujenga Rama, akaenda akakaa Tirza.

222 Nya 16:6; 1 Sam 8:16,17; Yos 21:17; 1 Sam 7:6 Ndipo mfalme Asa akatangaza kwa Yuda pia; asiachiliwe mtu; nao wakayachukua mawe ya Rama na miti yake, aliyoijengea Baasha; naye mfalme Asa akajenga kwa vitu hivyo Geba wa Benyamini na Mispa.

23 2 Nya 16:12; Zab 90:10; Mhu 12:1 Na mambo yote ya Asa yaliyosalia, na nguvu zake zote, na yote aliyoyafanya, na miji aliyoijenga, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda? Lakini alipokuwa mzee alikuwa na ugonjwa wa miguu.

241 Fal 22:41-43; 2 Nya 17:1; Mt 1:8 Asa akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze mjini mwa Daudi baba yake. Na Yehoshafati mwanawe akatawala mahali pake.

Nadabu atawala Israeli

25Nadabu mwana wa Yeroboamu alianza kutawala juu ya Israeli, mwaka wa pili wa Asa mfalme wa Yuda, akatawala juu ya Israeli miaka miwili.

261 Fal 12:30 Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akaiendea njia ya baba yake, na kosa lake alilowakosesha Israeli.

27 1 Fal 14:14; Yos 19:44; 21:23; 1 Fal 16:15 Basi Baasha wa Ahiya, wa ukoo wa Isakari, akamfanyia fitina; Baasha akampiga huko Gibethoni ulio wa Wafilisti; kwani Nadabu na Israeli wote walikuwa wakiuhusuru Gibethoni.

28Kum 32:35 Mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda Baasha akamwua, akatawala mahali pake.

291 Fal 14:10,14; Ayu 18:13-21; Zab 21:10; 37:28,38; Isa 14:20 Ikawa mara alipotawala, akawapiga nyumba yote ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu mwenye pumzi yeyote, hata alipomharibu sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa mtumishi wake Ahiya, Mshiloni;

30kwa sababu ya makosa yake Yeroboamu aliyoyakosa, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli; kwa sababu ya chukizo lake alilomchukiza BWANA, Mungu wa Israeli, hata kumghadhibisha.

31Basi mambo yote ya Nadabu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Israeli?

32Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli siku zao zote.

Baasha atawala Israeli

33Katika mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya alianza kutawala juu ya Israeli wote huko Tirza, akatawala miaka ishirini na minne.

341 Fal 12:28,29; 13:33; 14:16 Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA akaiendea njia ya Yeroboamu, na kosa lake ambalo kwa hilo aliwakosesha Israeli.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help