1Msingi wake upo
Juu ya milima mitakatifu.
2BWANA ayapenda malango ya Sayuni
Kuliko maskani zote za Yakobo.
3 Isa 60:1 Mambo makuu yanasemwa kukuhusu,
Ee Mji wa Mungu.
4Nitataja Rahabu na Babeli
Miongoni mwao wanaonijua.
Tazama Filistia, na Tiro, na Kushi;
Wanasema, Huyu alizaliwa humo.
5 Eze 48:35; Mt 16:18 Naam, kuhusu Sayuni yatasemwa,
Huyu na huyu alizaliwa humo.
Na Yeye Aliye Juu
Atauimarisha.
6 Zab 22:30; Isa 4:3; Yer 3:19; Eze 13:9 BWANA ataweka kumbukumbu, awaandikapo mataifa,
Huyu alizaliwa humo.
7Waimbao na wachezao ngoma na waseme,
Visima vyangu vyote vimo mwako.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.